Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




SEHEMU ILIYOKOSEKANA YA UNABII WA BIBLIA
IMEANGAZIWA KWETU LEO

A MISSING PIECE OF BIBLE PROPHECY
ILLUMINATED FOR US TODAY
(Swahili)

na Dr. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Jioni ya, Septemba 22, 2019
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Evening, September 22, 2019

“Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho....” (Danieli 12:4).

“Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje? Akasema, Enenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho” (Danieli 12:8, 9).


Nabii Danieli hakuelewa kinaganaga kuhusu “nyakati za mwisho.” Tumeambiwa wazi, katika mstari wa 8, “Nami nikasikia, lakini sikuelewa.” Kisha Mungu akamwambia Danieli, “maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho” (Danieli 12:9).

Danieli aliyaelewa maneno ya ule unabii. Lakini hakuelewa jinsi matokeo ya nyakati za mwisho yatakavyo kuwa. “Maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho” (Danieli 12:9). Aliyapokea yale maneno kwa kuongozwa na Mungu. Lakini hakufafanuliwa kuhusu maana yake. Kufafanuliwa kwa yale maneno hakungetendeka hadi “wakati wa mwisho.” Tunapoendelea kukaribia mwisho wa wakati huu, kutakuwa na ongezeko la ufahamu wa unabii.

Ninakumbuka vyema niliposikia mara ya kwanza kuhusu “unyakuzi.” Mwalimu wangu alitwambia kwamba unyakuzi utatendeka kabla ya kile kipindi cha miaka saba ya dhiki kuu. Nilimuuliza mwalimu wangu ni wapi Biblia inafundisha kwamba unyakuzi utatendeka kabla ya dhiki. Hakuweza kunijibu. Hivyo, kwa miongo kadha nimekuwa na swali kuhusu unyakuzi wa “wakati wowote”, kabla ya miaka saba ya dhiki. Kisha nikagundua ya kwamba unyakuzi kabla ya dhiki ulienezwa na J. N. Darby, na ya kwamba Darby “aliupata” kutoka kwa msishana aliyekuwa na umri wa miaka kumi na tano aliyeitwa Margaret MacDonald, aliyekuwa mwenye haiba “aliyeota” kuhusu unyakuzi kabla ya dhiki. Kwa sababu fulani J. N. Darby alianza kuieneza habari ile. Baadaye ilienezwa na C. I. Scofield katika Biblia ya kujifundisha ya Scofield. Na huo sasa ndio mtazamo wa madhehebu mengi yanayochipuka ya Kiinjilisti.

Halafu Marvin J. Rosenthal alikiandika kitabu kinachoitwa Unyakuzi wa kanisa kabla ya gadhabu (Kilichochapishwa na Thomas Nelson, 1990). Ingawa sikubaliani na mambo yote yaliyoandikwa na Rosenthal, nafikiri alifungua mlango katika kuelewa vyema kuhusu ni lini “unyakuzi” utakapotendeka. Pata hicho kitabu ukisome kabla haujakosoa maoni ya Kasisi Rosenthal. Anafundisha ya kwamba “unyakuzi” utatendeka unapokaribia mwisho wa kipindi cha Dhiki, muda mfupi kabla ya Mungu kumimina gadhabu katika “Hukumu ya Vitasa”, inayopatikana katika Ufunuo sura ya 16. Hii ina maana kwangu – ina maana zaidi kuliko ile ambayo inaegemea ndoto ya tineja!

Kwa nini hii ina maana? Nitakujulisha ni kwa nini. Ikiwa unyakuzi utakuja kabla ya miaka saba ya Dhiki, Wakristo basi hawahitaji kufanya jambo lolote. Ni kuwa tu na umati kwa saa moja siku ya Jumapili! Hauhitaji kumfikia aliyepotea. Hauhitaji kujitenga na wasiomcha Mungu. Dhana hii uelekeza katika Wokovu rahisi (Bonyeza hapa usome kuhusu hilo).

Kichwa cha ujumbe huu ni, “Sehemu ya Unabii wa Biblia Uliokosekana Umeangaziwa kwetu leo.” Sehemu hiyo “iliyokosekana” ni ipi?” Ni “Uasi.” Nimekuwa nikisoma Unabii wa Biblia kwa zaidi ya miaka 50. Inanishangaza kabisa kwamba jambo muhimu kama hili la Uasi” limesahaulika sana katika wakati huu wetu. Katika deski yangu ninavyo vitabu vitatu vikuu vya unabii wa Biblia – vinavyozungumzia mambo muhimu katika unabii. Viliandikwa na watu wazuri na wanaomwogopa Mungu, watu ambao wanaweza aminika kwa mambo muhimu. Lakini kimoja cha hizi vitabu kina sehemu ya “Uasi”. Na “Uasi” ni jambo muhimu sana kwetu leo.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Tafadhali fungua II Wathesalonike 2:3. Hii ni tafsiri ya Mfalme Yakobo,

“Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu” (II Wathesalonike 2:3).

Hapa ni hilo andiko katika tafsiri nyingine,

“Mtu asiwadanganye kwa namna yo yote maana siku hiyo haitakuja kabla ya uasi kutokea kwanza na yule mwasi adhihirishwe, yule ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa” (II Wathesalonike 2:3, SNT).

“Uasi” unatafsiriwa “hē apostasia.” pia inatafsiriwa “kuanguka” katika tafsiri ya Mfalme Yakobo.

Dkt. W. A. Criswell alipata shahada ya uzamivu ya uchunguzi katika lugha ya Kiyunani kutoka Chuo cha Theolojia cha Baptisti ya Kusini kule Louisville, Kentucky. Dkt. Criswell kila wakati aliyaangalia maneno ya Kiyunani yaliyo katika Agano Jipya kwa makini. Dkt. Criswell alisema, “Kabla ya siku ya Bwana, kutakuwa na uasi unao onekana wasi hata kwa watu wanao kiri kwamba ni waumini. Katika nakala hii anaonyesha ya kwamba Paulo alikuwa anamaanisha uasi aina fulani.” Tukiyafahamu haya, tutayaelewa mambo mawili muhimu katika II Wathesalonike 2:3,


1. Kabla ya siku ya Bwana, uasi huu utatokea.

2. Kabla ya siku ya Bwana, Mpinga-kristo atakuwa “amedhihirishwa.”


Mambo haya mawili yatatendeka kabla ya Siku ya Bwana, ambayo ni dhiki na wakati wa gadhabu ya Mungu, katika mwisho wa kizazi hiki. Katika nadharia ya Unyakuzi kabla ya dhiki Wakristo wote watakuwa tayari wameenda. Na hii ndio sababu “uasi” hauhubiriwi kwa Wakristo wa kiinjilisti siku hizi, na hiyo ndiyo sababu hakuna sehemu ya “uasi” katika vitabu vingi vya Unabii wa Biblia siku ya leo!

Lakini ikiwa Marvin Rosenthal yuko sahihi, na yuko sahihi, basi tuko katika mwanzo wa “uasi” sasa hivi! Hii ina mwathiri Mkristo kwa namna gani siku ya leo? Katika “Ulimwengu wa Tatu” Wakristo wanateswa zaidi wakati huu kuliko wakati uliopita. Na katika “Ulimwengu wa Magharibi” tunapitia katika mashambulizi makali kutoka kwa Shetani na mapepo wake. Nabii Danieli aliambiwa mambo haya, lakini alisema, “siyaelewi.” Kisha Mungu akamwambia Danieli, “maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho” (Danieli 12:8, 9).

Yohana S. Dickerson ameandika kitabu kizuri kiitwacho, Mporomoko Mkuu wa Uinjilisti (Vitabu vya Baker, 2013). Dickerson anamnukuu Gabe Lyons, aliyesema,

Wakati huu haufanani na wakati mwingine wowote katika historia. Hali yake ya kipekee inahitaji jawabu halisi. Ikiwa tutashindwa kupeyana mwelekeo, tutapoteza kizazi kizima kwa utepetevu na ukosoaji...marafiki wetu wataendelea kupeperuka kwa aina nyingine za ibada...za muda mfupi, lakini za kupendeza (Wakristo wa baadaye, Doubleday, 2010, uk. 11; msisitizo ni wangu).

Jalada la kitabu cha Dickerson inasema,

“Kanisa la Marekani... linapungua.Vijana Wakristo wanaondoka. Mchango wetu unapungua...Utamanduni wa Marekani unageuka kwa haraka kuwa na ukatili na uadui. Tunawezaje kujiepusha na mporomoko mkubwa?”

Ingawa napenda sehemu ya kwanza ya kitabu cha Johana Dickerson, sikubaliani na mambo mengi katika sehemu ya mwisho, kuhusu jinsi ya kujitayarisha.

Katika kujitayarisha ni lazima tufahamu ya kwamba tuko, sasa hivi, katika mwanzo wa “uasi.” Ikiwa tutafikiria tutanyakuliwa kabla ya kuwa na taabu zaidi, hatutaweza kujiandaa kwa mambo yaliyo mbele.

Mchungaji Richard Wurmbrand alikuwa mhubiri mhijilisti aliyefungwa miaka 14 katika gereza za Wakomunisti, aliteswa kwa ajili ya Kristo kule Romania. Mambo aliyoyapitia katika jela yanazidi mateso ambayo yamewahai kujulikana na Wakristo katika Marekani. Panya walikula miguu yake usiku katika seli. Alipigwa. Vichocheo vilivyokuwa vyekundu kwa kupashwa moto vili muweka majeraha mabaya katika shingo yake na mwili. Alinyimwa chakula kiasi cha kuwa karibu kufa. Na maovu haya yaliendelea kwa miaka 14. Hili lilimfanya Mchungaji Warmbrand kuyatengeneza mafundisho aliyoyaita “elimu ya mateso,” yaani mafunzo kuhusu mateso. Alipokuja Marekani (kwa njia ya muujiza) alifundisha hitaji la kujiandaa kwa mateso katika makanisa mengi – likiwemo hili kanisa letu. Mchungaji Wurmbrand alifundisha ya kwamba Wakristo katika Marekani lazima wajiandae kwa mateso. Alisema, “Inabidi tufanye matayarisho sasa, kabla hatujafungwa gerezani. Ukiwa gerezani unapoteza kila kitu...hakuna chochote kinachobakia cha kufanya maisha ya kupendeza. Hakuna yeyote anayeweza kubaki imara ambaye hakujinyima raha za maisha.” (ilinukuliwa na Yohana Piper katika Taifa Liwe na Furaha, Vitabu vya Baker, 2020, uk. 10).

Dkt. Paulo Nyquist alisema, “Muwe tayari. Tamanduni zinapoendelea kubandilika katika nchi yetu, hivi karibuni tutakuwa na pingamizi kwamba tuache kuishi kama inavyofundishwa na Biblia...tutakapoitikia mateso” (J. Paulo Nyquist, Jiandae: Kuishi Sawasawa na Imani yako katika Tamanduni ambazo Ukinzani Unaongezeka, Wachapishaji wa Moody, 2015, uk. 14).

SIKU ZA NUHU NI UASI

Yesu alisema,

“Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa atakaporudi Mwana wa Adamu. Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina. Nao hawakujua ni nini kitatokea mpaka gharika ilipokuja ika wakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa nitakapokuja mimi Mwana wa Adamu” (Matayo 24:37-39).

Waumini wengi wa mrengo wa Kiinjilisti ufikiria kwamba wakati wa Nuhu ulikuwa wakati wa mateso makubwa. Lakini kuna zaidi. Watu katika siku za Nuhu “walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina” (Mathayo 24:38).

Hivyo ndivyo inavyotendeka Marekani na mataifa ya Magharibi! Katika “Ulimwengu wa Tatu” kuna mateso mengi. Nchi kama Uchina kuna ufufuo wa kweli. Lakini si katika Marekani na Magharibi! Hapa watu wanajishughulisha na mali. Walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa. Haya yanaonekana mambo ya kawaida unapoyafanya. Lakini kuna zaidi. Hili ndilo jambo wanalolitilia maanani katika maisha yao – “wakila na kunywa, wakioa na kuolewa.” Walifikiria haya ndiyo mambo wanayostahili kuyafanya katika maisha yao! Kitovu cha maisha yao haikuwa Mungu! Yalikuwa mali yanayopatikana katika maisha ndiyo yaliyokuwa na umuhimu kwao!

KANISA LA LAODIKIA NI PICHA YA MAKANISA KATIKA MAREKANI NA MAGHARIBI

Yesu alisema,

“Kwa malaika wa kanisa la Laodikia andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aitwaye Amina, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa vyote alivyoumba Mungu. Nayajua matendo yako; kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali kama ungalikuwa baridi au moto. Basi, kwa kuwa wewe ni vuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu. Unajigamba ukisema, ‘Mimi ni tajiri , nimefanikiwa wala sihitaji kitu cho chote.’ Lakini hutambui kwamba wewe ni mnyonge, mtu wa kuhurumiwa, maskini, kipofu; tena wewe ni uchi. Kwa hiyo ninakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosaf ishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri; na mavazi meupe ili upate kuvaa, ufiche aibu ya uchi wako. Ujinunulie pia mafuta uyapake macho yako ili upate kuona. Wote niwapendao, ninawakaripia na kuwarudi. Kwa hiyo fanya bidii, utubu na kuziacha dhambi zako” (Ufunuo 3:14-19).

Hii ni picha ya kanisa lililoasi. Ni kanisa lililovuguvugu ambalo, “si baridi wala si moto” (Ufunuo 3:16). Ni kanisa lililojaa watu ambao hawajaongoka (Ufunuo 3:17). Ni kanisa lililokataa kutubu (Ufunuo 3:19).

Tumepitia kupasuka kwa kanisa mara mbili katika kipindi cha miaka 40 iliopita. Na kila wakati ni wale watu waliotaka kuwa “vuguvugu” ndio walioondoka. Wote wawili wakawa “vuguvugu” katika kufikia nafsi zilizopotea. Wote wawili walikataa kuwa Wakristo wa kweli. Jambo lililofanya watu waondoke kutoka kwetu, kwao, lilikuwa kwamba tuko “wangalifu sana” na wangalikuwa na wakati wa “burudani” ikiwa wengelituacha. Lakini mara zote mbili walishindwa kuwa na kanisa “linaloshamiri”. Wote wawili waligundua (kwa kuchelewa) kwamba hata watu wao wenyewe hawangewekwa katika mazingira yalio vuguvugu. Mwishowe wote wawili walifeli. Yesu alisema, “nitakutapika utoke kinywani mwangu” (Ufunuo 3:16). Hawakutaka kujitenga na Ulimwengu, hivyo ulimwengu hukaingia ndani yao, mwili, na Shetani. Hawakutaka kuwa wapiganiaji wa misingi halisi ya maandiko, na kwa haraka wakawa vuguvugu wa madhehebu mapya ya Kiinjilisti! Katika hali ya kiroho kwa haraka wakawa nusu hai – au wabaya zaidi!

Jiulize. Ingekuwa watu walioondoka na Chan walikuwa China, wangelikaa katika kanisa la siri, ama wangejiunga na makanisa yanayoungwa mkono na ukomunisti ya“Ubinafsi-Tatu”? Unalijua jawabu! Tayari unalijua jawabu! Wangekimbilia makanisa ya Kikomunisti. Kwa nini? Kwa sababu hawakutaka Ukristo wa kweli. Vinywa vyao vilikuwa na njaa ya “kanisa”ororo jipya-la kiinjilisti. Na hiyo ndiyo mwasi Chan aliwapa! ”Kanisa” ororo jipya-la kiinjilisti. Na unajua hilo! Tayari unalijua!!! Siwambii jambo lolote jipya!!!

Nitatamatiza ujumbe huu na ufafanusi wa uasi katika makanisa mapya ya-kiinjilisti ya siku hisi,

“Lakini fahamu jambo hili: kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, watukanaji, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio na utakatifu; wasio na ubinadamu, wasiopenda kusuluhishwa, wachonganishi, walafi, wakatili, wasiopenda mema; wasaliti, wasiojali kitu, waliojaa majivuno, wapendao anasa badala ya kumpenda Mungu. Hao ni watu ambao kwa nje wataonekana kuwa wana dini, huku wakikana nguvu ya imani yao. Jiepushe na watu wa jinsi hiyo.” (II Timotheo 3:1-5).

“Wao humsikiliza kila mtu lakini hawawezi kutambua kweli” (II Timotheo 3:7).

“Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya kumcha Mungu ndani ya Kristo Yesu watateswa” (II Timotheo 3:12).

“Hubiri Neno; lisisitize wakati ufaao na wakati usiofaa; sadik isha, kemea, na kuonya kwa uvumilivu mkuu na mafundisho thabiti. 3 Maana wakati unakuja ambapo watu hawatavumilia kusikia mafund isho yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajilundi kia walimu tele watakaowaambia yale ambayo masikio yao yanatamani sana kuyasikia. 4 Watakataa kabisa kusikia kweli na watageukia hadithi za uongo. 5 Bali wewe uwe imara, kati” (II Timotheo 4:2-5).

“Kwa sababu Dema, kwa kuu penda ulimwengu huu wa sasa,” (II Timotheo 4:10).

“Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na wote wanaoleta mafara kano na vipingamizi kinyume cha mliyopokea. Waepukeni. Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno matamu ya kudanganya, hupo tosha mioyo ya watu wanyofu” (Warumi 16:17, 18).

Kaka zangu na dada zangu wapendwa, nabii Danieli hakuyaelewa kwa kina mambo niliyowahubiria usiku wa leo. Lakini shukuru Mungu kwamba alimwinua Mwanamisheni kwa jina Marvin Rosenthal aliyezungumzia hili jambo na kutupa “kuelewa upya kuhusu unyakuzi. Thiki na Kuja mara ya Pili” kwa Yesu (Jalada ya Unyakuzi wa Kanisa Kabla ya Thiki, kilichochapishwa na Thomas Nelson, 1990).

Ndio, tuko sasa katika mwanzo wa uasi mkuu wa nyakati za mwisho. Ndio, tutapitia mateso, kama wanavyo pitia watu wa China, kama alivyopitia Richard Wurmbrand, kama wanavyo pitia watu katika “Ulimwengu wa Tatu”. Lakini wanaompenda Kristo watapata ushindi mwishowe, maana Yesu alisema,

“Kwa kuwa umeshika agizo langu la kustahimili kwa subira, nitakulinda wakati wa ile dhiki itakayokuja duniani pote kuwajar ibu waishio ulimwenguni. Ninakuja upesi. Shika sana kile ulicho nacho asije mtu akachukua taji yako. Atakayeshinda nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo kamwe. Na nitaan dika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wake Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unakuja kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Pia nitaandika juu yake jina langu jipya. Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anay aambia makanisa” (Ufunuo 3:10-13).

Tafadhali simama na huimbe beti 1, 2 na 4 za “Mimi ni Askari wa Msalaba?”

Mimi ni askari wa msalaba, Mfuasi wa Mwana Kondoo,
Na sitaogopa kujitambulisha na kusudi lake, Au nionee haya Jina lake?

Lazima nibebwe angani na vitanda vya maua ya starehe,
Wakati wengine walipigania kushinda thawabu, Na kungoa nanga katika bahari ya umwagikaji wa damu?

Hakika lazima nipige vita, ikiwa nitatawala; Niongeze ujasiri, Bwana;
Nitastahimili taabu, nitavumilia uchungu, Nikisaidiwa na Neno Lako.
   (“Mimi ni Askari wa Msalaba?” na Dkt. Isaka Watts, 1674-1748).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.