Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




JINSI PETRO ALIPATA KUWA MWANAFUNZI

Maandishi ya Dkt. Christopher L. Cagan;
Yaliyohubiriwa na Dkt. R. L. Hymers, Jr.
Katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Jioni ya, Septemba 1, 2019
Text by Dr. Christopher L. Cagan;
preached by Dr. R. L. Hymers, Jr.
at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Evening, September 1, 2019

“Mmojawapo wa hao wanafunzi wawili waliomfuata Yesu baada ya kusikia maneno ya Yohana, alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro. 41 Mara baada ya haya Andrea alikwenda kumtafuta ndugu yake akamwambia, “Tumemwona Masihi,” yaani Kristo. 42 Andrea akampeleka Simoni kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana; sasa utaitwa Kefa.” Tafsiri ya Kefa kwa Kigiriki ni Petro, maana yake ‘Mwamba’” (Yohana 1:40-42).


Hii ndio mara ya kwanza ya Petro kukutana na Yesu. Jina lake la asili lilikuwa Simoni. Yesu alimpa jina “Petro,” linalomaanisha “mwamba.” Andrea alikuwa ndugu yake. Petro alikuwa mvuvi. Andrea na Petro waliishi katika kijiji ambacho hakikuwa mbali na Ziwa la Galilaya, mahali ambapo walifanya kazi yao ya uvuvi. Maisha yalikuwa magumu, maana uvuvi ni kazi inayoitaji utumie nguvu za mwili, ilikuwa kazi ngumu. Petro alikuwa na mke kwa sababu Yesu alimponya mama mkwe wake. Petro alikuwa na miaka kama thelathini hivi wakati ambapo alikutana na Yesu. Umri wake ulizidi wa wanafunzi wengine.

Wavuvi waliokuwa katika ziwa la Galilaya walikuwa shupavu. Uvuvi ulikuwa hasa kazi iliyohitaji nguvu za mwili. Mambo waliokutana nayo yaliwaweka woga, kwa sababu dhoruba kali zilikuwa zinatokea gafla katika Ziwa la Galilaya. Dhoruba hizo zingeingia katika mashua zao ndogo na kuwafanya wazame.

Petro hakuwa mfarisayo. Kwa kuwa alikuwa Myahudi wakati mwingi alienda katika sinagogi. Hakushikamana na desturi sana, kama vile Mafarisayo. Lakin alilijua jambo ambalo wavuvi wengine hawakulijua, Petro alijua moyoni mwake kwamba ni mwenye dhambi. Baadaye alimwambia Yesu, “Ondoka mbele yangu, ee Bwana, kwa kuwa mimi ni mwenye dhambi!” (Luka 5:8).

Hivyo, Petro hakuanza kama mtu wa dini, au Mkristo mzuri. Alikuwa na tabia ya ukali. Alihitaji kuwa mkali ili awe mvuvi. Hakuwa kama “mtu wa kanisa” aliyepokea mafundisho kamili” Alitumia lugha mbaya na alikuwa mwenye hasira. Alikuwa mwenye dhambi aliyefanya makosa mengi.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Sasa fikiria kuhusu mtu unayejaribu kumfikia kwa ajili ya Kristo. Kama Petro, hajawezeshwa na kupewa mafunzo kama “mtu wa kanisa.” Haelewi ni kwa nini aje katika mikutano ya kanisa. Anafikiria ni jambo nzuri kucheza michezo ya video kwa masaa mengi, ama kuwa katika ushirika wa marafiki waliopotea. Watu wote anaowajua anafikiria wako kama yeye. Ana dhambi zake. Ana mafikira yake mabaya. Ana matatizo yake. Hautaweza kumleta kwa Kristo kwa kubishana na yeye. Badala yake, mwambie kuhusu Yesu. Mwambie yale Yesu alikutendea. Fanya urafiki naye. Litakuwa wazo jema kuja naye kanisani. Petro hakuwa amefundishwa, na vilevile watu waliopotea katika Ulimwengu.

Nduguye Andrea alimwambia Petro kuhusu Yesu. “Mara baada ya haya Andrea alikwenda kumtafuta ndugu yake akamwambia, “Tumemwona Masihi,” yaani Kristo.” (Yohana 1:41). Petro hakufanyika mwanafunzi mara ile ya kwanza aliposikia kuhusu Yesu.

Hii ni ya muhimu sana. Katika insha inayohusu “maamuzi,” Dkt. A. W. Tozer anaeleza wasi kwamba kumfanya mtu aseme “ombi la mwenye dhambi” kwa kawaida hawafanyiki Wakristo wa kweli, wanafunzi wa kweli. Petro hakufanya “uamusi” mara ya kwanza aliposikia kumhusu Yesu. Ndio, Petro alivutiwa. Alitaka kusikia zaidi. Lakin haikuwa hadi baadaye, baada ya Yohana Mbatizaji kukamatwa, ndipo Petro aliamua kumfuata Yesu kama mwanafunzi.

“Yohana mbatizaji alipokamatwa na kutiwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya akaanza kutangaza Habari Njema za Mungu, akisema, ‘Wakati umefika: Ufalme wa Mungu umewasili. Tubuni, muamini Habari Njema.’ Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa la Galilaya alimwona Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa kutumia nyavu; ndugu hawa wawili walikuwa wavuvi. Yesu akawaambia, ‘Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.’ Wakaacha nyavu zao mara moja wakamfuata Yesu” (Marko 1:14-18).

Kila mtu unayejaribu kumwongoza kwa Kristo – wakati fulani ataamua ikiwa anataka kuwa mwanafunzi wa Kristo au la. Haya ni mapambano. Hii ni vita. Bado hajaamua anapoendelea kuja kanisani pamoja nawe kwa majuma kadha ama miezi kadha. Ni vita vinavyoweza kuendelea kwa miezi au miaka.

Kwa kutojua haya ndiko kunamfanya Kreighton Chan kuwa hafai katika uinjilisti. Yeye, kama walivyo wengi wanao amini maamuzi, wanafikiria “wamebobea” wakati ambapo wanaelewa tu juujuu “ukweli” kuhusu Injili. Wanaoamini maamuzi kama Kreighton na Waldrip uwafanya watu wapya kwenda “mbali” kwa muda mfupi. Hawafahamu ya kwamba kutafuta nafsi zilizo potea ni vita vinavyoendelea. Na hiyo ndiyo sababu kutafuta nafsi zilizopotea kwa kweli uhitaji hekima: “Na yule anayeziteka nafsi ni mwenye hekima” (Methali 11:30). Andiko hilo pia linaweza tafsiriwa, “Aliye mwenye hekima uziteka nafsi.” Dkt. A. W. Tozer kwa hekima alisema,

“Kwa kujaribu kulazimisha wokovu mara moja badala ya mara mbili, wana harakati wa Ukristo wa mara hiyo hiyo wamekosa kuzingatia sheria ya hatua kwa hatua katika hali yote ya maumbile. Wanapuuza athari ya kutakaswa kupitia mateso, kuubeba msalaba na kutii kwa vitendo. Wanaepa lile hitaji la mafunzo ya kiroho, umuhimu wa kuwa na tabia nzuri za dini na hitaji la kushindana na dunia, shetani na mwili” Upungufu wa ‘Ukristo wa Gafla’).

Petro alijaribiwa kulipotokea “mgawanyiko mkubwa wa kanisa.” Wengine walitoroka. Lakini Petro aliamua kukaa. Aliamua hataenda pamoja na wengine.

“Kutokana na hayo, wengi wa wafuasi wake walirudi nyuma wasiandamane naye tena. Basi, Yesu akawauliza wale kumi na wawili, ‘Je, nanyi pia mwataka kwenda zenu?’ Simoni Petro akamjibu, ‘Bwana, tutakwenda kwa nani? Wewe unayo maneno yaletayo uzima wa milele. Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu.’” (Yohana 6:66-69).

Yesu aliwaambia wale thenashara, “Je, nanyi pia mwataka kwenda zenu?” “Simoni Petro akamjibu, "Bwana, tutakwenda kwa nani? Wewe unayo maneno yaletayo uzima wa milele” (Yohana 6:67, 68). Kuna mambo mawili muhimu katika kifungu hiki.

1. Walio ondoka hawakusikika tena! Nimegundua katika miaka yangu 61 katika huduma kwamba wanaoondoka kunapotokea mgawanyiko wa kanisa hawawezi kuwa wanafunzi wenye nguvu. Sijawahi kumwona mmoja aliyefanyika mwanafunzi mwenye nguvu!

2. Kama Petro angelienda na ule “mgawanyiko” pengine angeongoka.

“Watu hao walitoka kati yetu, lakini hawakuwa wa kundi letu. Kama wangekuwa wa kundi letu, wangeendelea kuishi pamoja nasi; lakini waliondoka ili iwe wazi kuwa hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kundi letu” (I Yohana 2:19).

“Waliwaambieni kwamba, ‘Katika siku za mwisho, watatokea watu watakaowadhihaki, watu wafuatao tamaa zao mbaya.’ Watu hawa ndio wanaosababisha mafarakano, watu wafuatao tamaa za dunia, wasio na Roho wa Mungu” (Yuda 18, 19).

Wale ambao huondoka udhihirisha kwamba hawajajua ukweli wa uanafunzi wa Wakristo. Kuwa mwanafunzi, mwongovu kamili, ni zaidi ya kukariri vifungu kadha vya Biblia, au kuamini mafundisho kadha. Uanafunzi uhusisha uamuzi wa kusalia; na hakuna maana ya kuondoka, kwa sababu hakuna chochote cha dhamana “kule nje.” Petro aliyaona mambo haya – lakini bado hakuwa ameongoka!

Nafikiria unaweza kuona ya kwamba kutafuta nafsi iliyo potea ni mradi! Si tu kupata jina au kumpata mtu atakayesema ombi la toba. ni mapambano yanayoendelea kwa ajili ya nafsi ya mtu aliye hai!

Uongofu na uanafunzi ni zaidi ya kuangaziwa kuhusu Yesu ni nani!

“Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani? Simoni Petro akamjibu, ‘Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.’ Na Yesu akamwambia, ‘Umebarikiwa, Simoni mwana wa Yona, kwa maana si mwanadamu aliyekufunulia hili, bali ni Baba yangu aliye mbinguni’” (Mathayo 16:15-17).

Mungu Baba alimfunulia (alimwangazia) Petro kuhusu Yesu ni nani. Mungu alimfunulia Petro Yesu hasa alikuwa nani. Lakini Petro bado hakuwa ameongoka!!! Watu wengi ufikiria kuwa alikuwa ameongoka wakati huo. Lakini wamekosea!

Kwanzia wakati ambapo Yohana alimwonyesha Petro Yesu hasa alikuwa nani – wakati huo Petro alianza kuikataa Injili!!!

“Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi kutoka kwa wazee, makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na siku ya tatu atafufuliwa. Petro akamchukua kando akaanza kumkemea akamwambia, ‘Mungu apishie hayo mbali! Jambo hili halitakupata kamwe!’ Lakini Yesu akageuka akamwambia Petro, ‘Toka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo hayo si ya Mungu bali ya binadamu’” (Mathayo 16:21-23).

Petro aliikataa Injili. Alimkemea Yesu aliposema anaelekea Msalabani na atafufuliwa kutoka kwa wafu. Alikataa Injili! Hivyo, mtu anaweza kuwa mfuasi wa Yesu kwa miaka kadha na bado awe anangangana na kupigana. Kabisa!

Petro alijivuna kwamba alikuwa Mkristo hodari. Usiku ule kabla ya kusulibiwa kwa Kristo, Petro alimwambia,“Hata kama itabidi nife pamoja na wewe, sitakukana.”(Mathayo 26:35). Bado masaa machache baadaye Petro alimkana Yesu mara tatu!

Petro alikuwa bado hajaongoka! Alimwacha Yesu alipotiwa nguvuni pale Gethsemane. Alimkataa Kristo kwa sauti mara tatu. alikuwa mwanafunzi pamoja na wengine – lakini mapambano yake yalikuwa hayajaisha bado. Bado hakuwa ameongoka. Hakuwa ameingia katika wokovu!

Ni pale Yesu alipofufuka kutoka kwa wafu ndipo Petro mwishowe aliongoka. Imerekodiwa katika Yohana 20:22,

“Jumapili hiyo jioni, wakati wanafunzi walikuwa pamoja huku milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwato kea! Akasimama kati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” Baada ya kusema haya, aliwaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi walifurahi sana walipomwona Bwana! Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama Baba alivyonituma, mimi pia nawatuma ninyi.” Na alipokwisha kusema haya akawavuvia pumzi yake akawaambia, ‘Pokeeni Roho Mtakatifu’” (Yohana 20:19-22).

Mfasiri Yohana Ellicott alituambia ya kwamba Mtume Yohana “alikumbuka jinsi ushawishi wa wakati huo uliwaelekeza katika maisha yao kua viumbe vipya vya kiroho, ambapo waliitwa kutoka kwa wafu kuingia katika uzima” (Mafafanusi ya Ellicott kwa Biblia Nzima). Na bila shaka, Dkt. J. Vernon McGee alisema huu ndio wakati petro alifanywa upya, akazaliwa mara ya pili, usiku ule Yesu alifufuka kutoka kwa wafu! (Tazama Kupitia Biblia katika Yohana 20:22).

Huo ndio wakati Petro alimwamini Yesu kikamilifu. Baadaye akawa Mtume shujaa ambaye alihubiri siku ya Pentekoste ambapo watu elfu tatu waliokoka. Baadaye alikufa kwa ajili ya Kristo badala ya kumkana. Lakini kabla ya hayo yote, Petro alipitia mwanzo usiokuwa wa kweli pamoja na kufeli, mapambano na ujuzi.

Basi unaweza kuona kwamba kuitafuta nafsi iliopotea ni jambo nzito na mapambano makali? Haiwezi tendeka kupitia simu ama ombi. Ni mapambano ya maisha kwa sababu ya uzima wa nafsi ya mwanamume au mwanamke. Itagharimu maombi yako. Itahitaji hekima. Itahitaji jitihada. Itachukua muda. Ikiwa utaweza kuipata nafsi moja iliopotea katika maisha yako yote, umebarikiwa. Umefanya kazi nyingi. Umefanya vyema. Ni ombi langu kwamba utawezeshwa kufanya hivyo.

Je! Hii inaonekana njia ndefu ya kufuata? Inaonekana kuwa ngumu na ndefu? Yeus alisema, “Lakini njia inayoongoza kwenye uhai ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo” (Mathayo 7:14).

Lakini wacha Petro mwenyewe atupe neno la mwisho katika ujumbe huu. Haya ndiyo maneno ya mwisho Petro mwenyewe aliyaandika kabla hajasulibishwa,

Lakini endeleeni kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu uwe kwake, sasa na hata milele! Amina” (II Petro 3:18).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.