Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.
Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.
Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.
KUTIWA MOYO NA MAONYO KATIKA DHIKI –
|
Yesu alisema, “Ulimwenguni mnayo dhiki.” Neno lililotafsiriwa “dhiki” ni neno la Kiyunani thlipsis. Lingetafsiriwa kuwa “shinikizo.” Kila mmoja anayo shinikizo fulani katika maisha yake. Lakini wakati mbaya wa shinikizo bado unakuja. Dhiki kuu ni ule muda wa miaka saba kabla Yesu ajashuka pale Mlima wa Mizeituni kutawala katika Ulimwengu katika haki. Sehemu mbaya zaidi katika dhiki kuu ni ile miaka mitatu na nusu ya mwisho. Katika ile miaka saba kabla ya kurudi kwa Kristo duniani, Mpinga Kristo atatawala ulimwengu. Biblia inaonyesha ya kwamba kila anayekuwa Mkristo atauawa au atateswa.
Mtume Yohana aliona maono ya nafsi za hawa Wakristo wa dhiki kuu wakiwa Mbinguni. Alisema,
“Nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao” (Ufunuo 6:9).
Alafu akaandika,
“Hao ndio wanaotoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.” (Ufunuo 7:14).
Miaka hii saba itakuwa mibaya zaidi kwa Wakristo kuliko wakati mwingine wowote katika historia. Yesu alisema,
“Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe” (Mathayo 24:21).
Ndio, kutakuwa na unyakuzi. Biblia inasema,
“Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” (I Wathesalonike 4:16-17).
Bado tusifikirie kwamba ahadi hii itatuponya tusipitie mateso siku ya leo, kabla ya dhiki kuu. Katika somo letu, Yesu alisema ya kwamba Wakristo watapitia mateso katika wakati huu.
“Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu” (Yohana 16:33).
+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +
MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.
+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +
Hebu tuangalie yale Yesu alisema hapa kwa uangalifu. Nitazungumzia sehemu ya pili ya hili andiko, alafu sehemu ya kwanza, na kisha sehemu ya mwisho.
I. Kwanza, “ulimwenguni mnayo dhiki.”
Yesu alisema haya kwa Wanafunzi wake, na hili jambo linahusu kila Mkristo katika enzi hii. Wakristo watakuwa na mateso halisi. Mtume Paulo aliandika,
“Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili…” (II Wakorintho 12: 7).
Hili linaonekana linaelekeza katika taabu Paulo aliyokuwa nayo katika macho yake. Hili linaonyesha ya kwamba Wakristo watapitia mateso halisi ya magonjwa, uchungu, na pia kifo cha mwili. Hatuepuki magonjwa katika miili na uchungu tunapokuwa Wakristo.
Wakristo pia watapitia mateso mengine na taabu katika ulimwengu huu wetu ulioanguka, na ulio na dhambi. Mtume Paulo alizungumzia Wakristo kupitia
“…Dhiki au shinda, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.” (Warumi 8:35-36).
Lakini aliashiria kwamba mateso haya “hayatatutenganisha na upendo wa Kristo” (Warumi 8:35a).
“Ulimwenguni mnayo dhiki” (Yohana 16:33).
Mitume wote waliuawa kwa sababu ya imani yao katika Kristo – isipokuwa Yohana –aliyetumbukizwa katika mafuta yaliyekuwa yakichemka, na kuwa na kovu katika maisha yake yaliyosalia. Wakristo katika enzi zote wameteseka kwa sababu ya imani yao. Kitabu cha wanaouawa au kuteswa kwa sababu ya imani yoa cha Foxe ni kitabu bora kinachoandika mateso ya Wakristo wafia dini katika historia. Dkt. Paulo Marshall alisema,
Katika misitu ya Marekani ya kati…makambi ya kufanyishwa kazi ya Uchina, jela za Pakistani, ghasia za India, na katika vijiji via Sudani waumini wengi wamelipia thamani ghali kwa kupitia mambo magumu kwa sababu ya imani yao (ibid., kurasa 160).
Katika nchi ya Sudani Wakristo wanafanywa kuwa watumwa. Katika nchi ya Irani wanauawa kisiri. Katika nchi ya Kuba wanatiwa gerezani. Katika nchi ya China wanapigwa hadi kufa. Katika zaidi ya nchi 60 katika ulimwengu Wakristo wanahangaishwa, wanadhulumiwa, wanateswa au kuuawa kwa sababu ya imani yao. Wakristo 200,000,000 ulimwenguni kote wanaishi kwa woga wa polisi wa siri, waangalifu, au kunyamazishwa na kutengwa na vyombo vya dola… mamia ya mamilioni ya Wakristo wanateseka kwa sababu ya kile wanachoamini (Paulo Marshall, Ph.D., Damu yao inalia, Neno, 1997, jalada la nyuma).
Hata hapa katika magharibi, Wakristo wa kweli wanabaguliwa na kukosewa heshima au wanahangaishwa na jamii ya wasioamini inayoendelea kuongeseka. Ukristo na Biblia unadhihakiwa katika madarasa ya vyuo. Wakristo wengi wanakosa kupandishwa vyeo, na wengine wanaondolewa kazini kwa sababu ya shauku yao ya kumwabudu Mungu makanisani mwao katika Siku ya Bwana. Hata watu wa jamii ambazo si Wakristo na Wakristo wa Kiinjilisti wapya na waliowadhaifu uwadharau Wakristo waaminifu. Kama alivyosema Yesu,
“Ulimwenguni mnayo dhiki” (Yohana 16:33).
II. Pili, “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu.”
Hii ni ahadi kwa wale walio “ndani ya Kristo.” “Ndani yangu.” Yeye ndiye chanzo cha amani ya ndani. Yesu alisema,
“Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo…” (Yohana 14:27).
Mtu anapomjua Kristo, huwa na amani iliyotulia ndani yake ambayo wengine katika ulimwengu hawana.
Mtu aliye “ndani” ya Kristo, na anayekabidhi matatizo yake kwa Mungu katika njia ya maombi, ana amani ya kipekee, ambayo Biblia inaiita “amani ya Mungu, ipitayo akili zote,” (Wafilipi 4:7). Ulimwengu hauwezi ukaelewa kwa nini Wakristo wanapitia mambo kama vile kukamatwa, kuteswa, kufungwa jela, na kuuawa – kama vile walivyo katika nchi nyingi katika ulimwengu siku ya leo.
Amani hii haimaanishi ya kwamba Mkristo hana mapambano ndani yake, matatiso kihisia, ama magonjwa katika mwili wake. Wakristo wengi wakiinjilisti katika Marekani wana tamaa ya mafanikio, mali, starehe, furaha, na kujifanikisha kibinafsi. Jambo hili linaweza kuonekana kama mzaha, kwa Mkristo Mchina anayesulibishwa akifudikizwa kwa sababu ya imani yake, au Mkuba Mkristo ambaye amezuiliwa katika kifungo kwa miaka mitano, ama Mkristo katika nchi ya Irani anayekabiliwa na kifo kwa sababu ya kumwamini Yesu.
Wakristo hawa wanaoteswa katika nchi za Ulimwengu wa Tatu wamekaribia zaidi kuelewa Yesu alivyomaanisha aliposema, “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu.” (Yohana 16:33). Ninafikiria wataelewa kwamba amani hii inazungumzia kule kuwa na utulifu wa ndani, unaotokana na kujua kwamba dhambi zao zimesamehewa, na kwamba Mungu anawajali.
Ninaenda kusoma II Wakorintho 11:24-28. Sikiliza ninapokwambia yaliyompata Mtume Paulo. Alisema,
“Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivujikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi. Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote.” (II Wakorintho 11:24-28).
Ni vipi Paulo angezungumzia kuwa na amani kwa mazingira ya namna hii? Bado alifanya hivyo. Paulo alipeyana jibu katika Wafilipi 4:6, 7.
“Msijisumbukie kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu” (Wafilipi 4:6-7).
Paulo alipitia dhiki nyingi na mateso, na bado hapa alizungumzia kuhusu “amani ya Mungu, ipitayo akili zote.”
III. Tatu, “jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.”
Unaweza shangaa ikiwa utaweza au hautaweza kupitia majaribu na dhiki za maisha. Vijana katika vyuo vya kiulimwengu lazima wawe pale darasa baada ya darasa, mahali ambapo Biblia na Wakristo wanashambuliwa kwa mambo machungu, kuvunjiwa heshima na kudhihakiwa. “Ninaweza endelea kweli, na nibaki nikiwa Mkristo?” mwanafunzi wa chuo ufikiria. “Ninaweza kuyapitia mateso haya? Ninaweza kufaulu watu wanapoinuka kinyume nami? Ninaweza vumilia wakati ambapo ninawoga– na sina imani nyingi?”
Leo Wakristo wa kweli wanadhihakiwa kuwa washupavu. Watu watasema unafanya mambo kupindukia kwa sababu ya Yesu. Wanakualika kwa dini rahisi ya muda wa saa moja tu Juma pili asubuhi, au kusiwe na kanisa kabisa. Wanasema utakuwa na furaha ikiwa utaacha kumfuata Kristo. “Hakuna maana ya kuubeba msalaba. Hakuna maana ya mateso au maumivu, wanasema hivyo. “Sahau hayo yote. Achana na hayo mambo na uwe jinsi tulivyo.” Wanakushurutisha. Kama vile Yesu alivyosema, “Ulimwenguni mnayo dhiki.”
Lakini Kristo anasema, “jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.” Sikiliza ninaposoma Warumi 8:35-39.
“Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shinda, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 8:35-39).
Unapokuja kwa Kristo, anachukua usukani. Atakushikilia na hatakuachilia uende. Unapokuja kwa Kristo, hauhitaji kumshikilia. Yeye ukushikilia! Kuanzia wakati wa uongofu wako, milele uko salama katika Kristo. Ukweli kwamba kuna watu milioni 200 katika Ulimwengu wa Tatu walio tayari kuteseka kwa sababu ya imani yao ya Kikristo ni jambo linaloonyesha kwamba Kristo uwashikilia wafuasi wake, na hatawaachilia wapotee bila tumaini la Mbinguni. Kuja kwa Kristo, na anafanya wokovu wote, na kule kuhifadhi kwote! Kama alivyoimba Bw. Ngann kabla ya mahubiri,
Nafsi iliyomwegemea Yesu imepata pumziko,
Sitawahi, Sitawahi kumwacha kuungana na maadui wake;
Nafsi hiyo, ingawa kusimu yote itajaribu kuitikisa,
Sitawahi, hapana kamwe, hapana kamwe sitamwacha.
(“Msingi Ulio Thabiti,”
‘K’ ‘katika mchanganyiko wa nyimbo za Rippon,’ 1787).
Kichwa cha mahubiri haya ni “Kutiwa Moyo na Maonyo katika Dhiki – Sasa na Wakati Ujao.” Nimewatia moyo usiku huu. Lakini pia ni lazima niwape neno la onyo. Mateso tunayoyapitia sasa ni madogo mno unapoyalinganisha na mateso watu wanayoyapitia sehemu zingine. Katika Ulimwengu wa tatu Wakristo wanapigwa, wanafungwa jela, wanateswa na kuuawa kwa kumwamini Yesu. Maisha yetu hapa Marekani ni kama wakati wa mapumziko unapolinganisha na vile maisha yalivyo huko. Katika siku za usoni inaweza kuwa vigumu kuwa Mkristo hapa. Shinikizo itakuwa mbaya zaidi. Unaweza poteza kazi yako, nyumba yako, na pesa zako kwa kuwa Mkristo wa kweli aliyejitolea. Inatendeka nchi zingine sasa hivi. Marafiki zako na jamaa zako wanaweza kukugeuka. Alipokuwa akizungumzia kuhusu dhiki, Yesu alisema, “Na ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe; na baba atamsaliti mtoto, na watoto watashambulia wazazi wao, na kuwafisha. Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye atakayeokoka” (Marko 13:12, 13). Inatendeka katika nchi zingine sasa hivi. Usishangae ikiwa watu watakukataa hata kabla ya hiyo miaka saba.
Nabii Yeremia alisema, “Ikiwa umepiga mbio pamoja na hao waendao kwa miguu, nao wamekuchosha, basi wawezaje kushindana na farasi? Na ujapokuwa katika nchi ya amani u salama, lakini utafanyaje hapo katika kiburi cha Yordani?” (Yeremia 12:5). Ndio, unapitia mateso aina fulani kwa sasa. Lakini ikiwa hauwezi faulu katika shinikizo ndogo za leo, utafanyaje mambo yatakapokuwa mabaya zaidi? Ikiwa hautaishi maisha ya Ukristo wakati huu unaofanana na likizo, utafanyaje dhoruba itakapokuja? Ninakusihi huwe Mkristo mwenye nguvu sasa. Ikiwa utafanya hivyo sasa utakuwa Mkristo mwenye nguvu wakati ujao. Nilifikiria hayo nilipokuwa Mkristo mchanga niliposoma kitabu cha Mchungaji Richard Wurmbrand, Kuteswa kwa ajili ya Kristo. Hakikuwa tu kitabu cha kusoma. Ni kitabu kilichobadilisha maisha yangu. Kuwa Mkristo kila wakati si likizo. Inaweza kuwa vigumu. Ni vigumu. Ndio, “lakini jipeni moyo” (Yohana 16:33). Lakini pia hesabu gharama (angalia Luka 14:28). Litakuwa jambo njema, kwa sababu utaishi na Kristo milele.
Na sasa ni lazima niongee na watu waliopotea walio hapa usiku wa leo. Yesu anakupenda. Alikufa msalabani kulipia dhambi zako. Alimwaga Damu yake kuziosha dhambi zako. Alifufuka toka kaburini kukupa uhai. Ukimwamini, utaokolewa milele. Lakini kumwamini Yesu si maneno machache. Kumwamini Yesu inamaanisha kumwamini Yesu. Ndio, kutakuwa na wakati mgumu. Ndio, unaweza kuteseka. Lakini ni jambo ambalo litakufaidi. Utamjua Yesu. Utaishi na Yesu milele ikiwa utamwamini. Ikiwa unataka kuzungumza nami kuhusu kumwamini Yesu, tafadhali njoo uketi katika safu mbili za kwanza za viti. Amina.
UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.
(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”
Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.
Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Jack Ngann:
“Mzingi Ulio Thabiti” (‘K’ ‘katika mchanganyiko wa nyimbo za Rippon,’ 1787).
MWONGOZO WA KUTIWA MOYO NA MAONYO KATIKA DHIKI – ENCOURAGEMENT AND WARNING IN TRIBULATION – Mahubiri yaliyoandikwa na Dkt. R. L. Hymers, Jr. “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu” (Yohana 16:33). (Ufunuo 6:9; 7:14; Mathayo 24:21; I Wathesalonike 4:16-17)
I. Kwanza, “ulimwenguni mnayo dhiki,” II Wakorintho 12:7;
II. Pili, “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu.” III. Tatu, “lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu,” |