Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




THIBITISHO TATU ZA KUFUFUKA KWA KRISTO

THREE PROOFS OF CHRIST’S RESURRECTION
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Jioni ya, Aprili 21, 2019

“Kwa maana mfalme anajua habari za mambo haya, nami naweza kusema naye kwa ujasiri, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua, kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni” (Mdo 26:26).


Katika sura ya 26 ya Matendo ya Mitume Luka ameandika ushuhuda wa uongofu wa Paulo kwa mara ya tatu. Sababu iliyomfanya Luka kuuandika mara tatu ni rahisi kuielewa. Kando na kifo na kufufuka kwa Kristo, hakuna tukio lingine katika historia ya Ukristo lililo na umuhimu kuliko uongofu wa Mtume Paulo.

Paulo alitiwa mbaroni kwa sababu ya kuhubiri,

“…mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambaye Paulo alikaza kusema kwamba yu hai” (Mdo 25:19).

Na sasa Paulo alisimama, mikono yake ikiwa imefungwa kwa mnyororo, mbele ya Mfalme Agripa. Agripa mwenyewe alikuwa Myahudi. Kwa hiyo Paulo alitetea mahubiri yake kwa mzingi wa unabii katika Agano la Kale unaozungumzia kufufuka kwa Kristo. Paulo pia alijitetea kwa kusema kwamba Mfalme Agripa tayari alijua kuhusu kusulibiwa na kufufuka kwa Kristo. Kusulibiwa na kufufuka kulikuwa kumetendeka kama miaka thelathini iliyokuwa imepita. Kila Myahudi alijua hilo, hata Mfalme Agripa. Hivyo Paulo alisema,

“…mfalme anajua habari za mambo haya, nami naweza kusema naye kwa ujasiri, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua, kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni” (Mdo 26:26).

“Jambo hilo halikutendeka pembeni.” Huo ulikuwa usemi wa kawaida wa Kiyunani siku hizo. Mafafanusi ya Dkt. Gaebelein yanasema,

Huduma ya Yesu ilijulikana mahali pengi katika Palestina, na Agripa angeweza kuwa aliisikia. kufa na kufufuka kwa Yesu kulishuhudiwa vya kutosha, na wakati huu Injili ya Ukristo ilikuwa imehubiriwa kwa miongo mitatu. Kwa kweli mfalme alijua mambo haya, “kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni” (Mafafanusi ya Expositor’s Bible, Frank E. Gaebelein, D.D., Mhariri Mkuu, Zondervan Publishing House, 1981, sehemu ya 9, uk. 554; maelezo katika Mdo. 26:25-27).

Watu wengi siku ya leo wanafikiria kwamba kufufuka kwa Kristo lilikuwa jambo la sirini lililojulikana tu na wavuvi wachache wajinga. Lakini hakuna lolote ambalo linaweza kuwa mbali na ukweli! Kufufuka kwa Kristo kulijulikana na kila Myahudi katika Israeli, na ni jambo ambalo lilizungumziwa ulimwengu wote wa Kirumi karibu miaka thelathini! Kufufuka kwa Kristo halikuwa jambo la siri!

“Kwa maana jambo hili halikutendeka pembeni” (Mdo. 26:26).

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Dkt. Lenski alisema,

Mambo yote yaliyosemwa juu ya Yesu yalitendeka katika mji mkuu wa taifa, na baraza pamoja na [Liwali wa Kirumi] Pilato walihusika, na Yesu alikuwa mtu aliyejulikana katika taifa, ambaye umaarufu wake ulijulikana na mataifa jirani. “Halikutendeka pembeni”… si jambo ndogo la sirini ambalo hakuna mtu alijua lolote kulihusu, lakini ni jambo lililokuwa kuu na muhimu, lilikuwa bayana na lilifika mbali, kwama [Mfalme] Agripa alilazimika kulitolea nadhari zake za kifalme (R. C. H. Lenski, D.D., Mafafanusi ya Matendo ya Mitume, Augsburg Publishing House, toleo la 1961, uk. 1053; maelezo kuhusu Mdo. 26:26).

“Kwa maana jambo hili halikutendeka pembeni” (Mdo. 26:26).

Maadui wa Kristo walikuwa na miongo mitatu ya kuthibitisha ya kwamba hakufufuka kutoka kwa wafu. Na bado walikuwa wameshindwa. Haikujalisha juhudi zao, maadui walishindwa kuthibitisha ya kwamba Yesu alikuwa katika wafu baada ya kusulibiwa kwake. Kufikia wakati ambapo Paulo aliongea na Mfalme Agripa, maelfu ya Wayahudi, na makumi ya maelfu ya Watu wa Mataifa, walikuwa wanatangaza, “Kristo amefufuka kutoka kwa wafu.”

Kufufuka kwa Yesu Kristo ndiyo msingi wa Ukristo. Ikiwa mwili wa Yesu haukufufuka kotoka kaburini, imani ya Ukristo haina msingi. Mtume Paulo mwenyewe alisema,

“Tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure” (I Wakorintho 15:14).

Si ajabu kwamba maadui wa Kristo walijaribu kwa bidii kukanusha kufufuka kwake! Na bado wote walishindwa. Si kubaliani na Greg Laurie kwa hoja nyingi, lakini nina kubaliana naye kuhusu kufufuka kwa Kristo. Greg Laurie alitoa sababu tatu kwa nini maadui wa Kristo walishindwa – ushahidi mara tatu wa kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu (Greg Laurie, Kwa nini ufufuo? Tyndale House Publishers, 2004, uk. 13-24). Naenda kuyafafanua.

“Kwa maana jambo hili halikutendeka pembeni” (Mdo. 26:26).

I. Kwanza, kaburi tupu.

Thibitisho la kwanza la kufufuka kwa Yesu ni kaburi tupu. Ukweli kwamba kaburi la Yesu lilikuwa tupu siku tatu baada ya kufa kwake ni thibitisho kuu la kufufuka kwake. Waandishi wote wane wa Injili wanakubaliana kwamba kaburi la Kristo lilikuwa tupu siku tatu baada ya kufa kwake. Washuhuda wengine wengi pia walithibitisha ukweli kwamba kaburi lilikuwa tupu.

Shambulizi la zamani kabisa la kufufuka kwa Kristo ni kule kusema kwamba mtu aliiba mwili wake. Makuhani wakuu

“…wakawapa askari fedha nyingi, wakisema, semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala…Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo” (Mathayo 28:12-15).

Lakini maneno haya hayakuwashawishi watu wengi. Akili ya kawaida itakwambia ya kwamba Wanafunzi hawakuiba mwili wake halafu wanjifanye kwamba amefufuka. Siku tatu zilizotangulia Wanafunzi walikimbilia maisha yao wakati Yesu alikamatwa na kusulibiwa. Haionekani ni ukweli kwamba watu hawa waliojawa na woga wangepata ushujaa wa kuiba mwili wa Yesu – halafu waanze kuhubiri kwa ujasiri ya kwamba alifufuka kutoka kwa wafu – jambo ambalo lilihatarisha maisha yao! Hapana, hilo ni jambo ambalo halingewezekana kabisa! Madai hayo hayaambatani. Wanafunzi walijificha katika chumba na mlango ulikuwa umefungwa, “kwa hofu ya Wayahudi” (Yohana 20:19). Walikuwa katika mshtuko. Hawakuamini kwamba angefufuka tena. Hakuna yeyote katika wafuasi wa Kristo ambaye alikuwa na imani au ushujaa wa kubishana na serikali ya Warumi iliyokuwa na nguvu na kuiba mwili wa Yesu. Huo ni ukweli wa kisaikolojia ambao hauwezi kupuuzwa.

Wachukiwa wengine, ambao wangeuiba mwili wa Kristo, ni maadui wake. Tatizo la dhana hiyo ni kwamba maadui wa Kristo hawakuwa na nia ya kupora kaburi lake. Makuhani wakuu na viongozi wengine wa dini walimuua Kristo kwa sababu alitishia desturi ya dini yao na jinsi walivyoishi. Jambo ambalo hawa watu hawangelipenda ni kwamba watu wafikirie Kristo yu hai tena! Hiyo ndiyo sababu hawa viongozi wa dini walifanya juhudi kuondoa jambo lolote kuhusu kufufuka kwake. Injili ya Mathayo inatwambia ya kwamba walienda kwa liwali wa Warumi, Pontia Pilato,

“Wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjaja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka. Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza” (Mathayo 27:63-64).

Pilato aliwaambia wachukue askari na walilinde kaburi “salama kadiri mjuavyo” – muwaweke askari kwa kaburi na mlilinde kadiri mwezavyo (Mathayo 27:65). Hivyo walilitia lile jiwe la kaburi muhuri na wakawaweka walinzi pale kulilinda (Mathayo 27:66). Ajabu, ilionekana kwamba hawa makuhani wakuu na viongozi wa dini walikuwa na matumaini ya kufufuka kwa Kristo kuliko walivyoamini Wanafunzi wake!

Ukweli ni kwamba wakuu wa dini walitumia taratibu za upeo kuzuia mwili wa Kristo usiibiwe. Walitaka kuthibitisha kwamba ahadi ya Kristo ya kufufuka kutoka kwa wafu ni uongo. Wakuu wa dini walifanya chochote walichoweza kuondoa uwezekano wowote wa habari kuenea kwamba Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. Kuiba mwili lingekuwa jambo la mwisho la maadui wake kulifanya. Lakini kama wangekuwa waliuiba mwili, bila shaka wangeutoa wakati ambapo Wanafunzi wake walianza kuhubiri kuhusu kufufuka kwake. Lakini maadui wa Kristo hawakuutoa mwili wake. Kwanini? Kwa sababu hawakuwa na mwili wa kutoa! Kaburi lilikuwa tupu! Kristo alikuwa amefufuka kutoka kwa wafu!

“Kwa maana jambo hili halikutendeka pembeni” (Mdo. 26:26).

Kaburi tupu ndilo thibitisho la kwanza la kufufuka kwa Kristo kutoka kwa wafu, lakini kuna mengi!

II. Pili, taarifa ya walioshuhudia.

Yesu aliposulibiwa, Wanafunzi wake walikosa tumaini. Imani yao iliharibiwa. Hawakuwa na tumaini kwamba watapata kumwona tena akiwa hai. Halafu Yesu akaja,

“akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu” (Yohana 20:19).

Wanafunzi walimwona akiwa hai mara kwa mara.

“Wale aliowathihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini” (Mdo. 1:3).

Mtume Paulo alisema kwamba Kristo aliyefufuka,

“alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja…baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake” (I Wakorintho 15:5-8).

Dkt. Yohana R. Rice alisema,

Angalia jinsi huo ushuhuda wa mamia ya watu halisi waliomwona Yesu baada ya kufufuka kwake ulivyokuwa na nguvu, wengine wao mara kwa mara katika kile kipindi cha siku arobaini! [Mdo. 1:3]. Sheria ya Biblia ilikuwa “katika kinywa cha washuhuda wawili au watatu.” Hapa kulikuwa na mamia ya washuhuda. Watu wengi wamehukumiwa kifo kwa ushuhuda wa mshuhuda mmoja au wawili.
     Ni watu kumi na wawili tu wanaohitajika ili jopo la majaji lifanye maamuzi muhimu katika kesi. Hapa kwa kweli washuhuda mamia walikubaliana ya kwamba Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Hakuna mtu hata mmoja aliyetokea kusema ya kwamba wameiona maiti yake baada ya siku ya tatu, ama kutofautiana na shuhuda hizo.
     Ushuhuda wa hao mashahidi – walioshuhudia kwa macho, mashahidi waliochangamana na mwokozi, waliomuguza, walioguza alama za misumari katika mikono yake na miguu yake, walimwona akila, waliozungumza na yeye kwa siku arobaini – Ushuhuda huo ulikuwa ushahidi ulio na nguvu kuliko kesi yeyote inayohitajika katika mahakama ya upeo ya Marekani ama mahakama nyingine yeyote katika ulimwengu…Ushahidi huu una nguvu kiasi kwamba ni wale tu hawataki kuuamini na ambao hawaangalii ushahidi wenyewe ndio wanaoukataa. Si ajabu kwamba Biblia inatangaza kwamba Yesu alijidhihirisha “nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteseka kwake,” Mdo’ 1:3 (Yohana R. Rice, D.D., Kufufuka kwa Kristo, Kimechapishwa na Sword of the Lord, 1953, uk. 49-50).

“Kwa maana jambo hili halikutendeka pembeni” (Mdo. 26:26).

Kaburi tupu, na mamia ya watu walioshuhudia kwa macho, ni thibitisho za nguvu za kufufuka kwa Kristo kutoka kwa wafu. Lakini kuna mengi zaidi.

III. Tatu, mateso ya Mitume.

Ikiwa kufufuka kulikuwa uongo ni kwa nini kila mmoja wa wale Mitume alipitia mateso makuu walipokuwa wakitangaza kufufuka kwake? Mitume hawakuendelea tu kuhubiri kufufuka kwa Kristo pekee, hata walikufa kuliko kukana! Tunaposoma historia ya kanisa tunapata kujua kwamba kila Mtume [isipokuwa Yohana – aliyeteswa na kupelekwa uhamishoni] alikufa kifo cha kutisha kwa sababu walihubiri kwamba Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. Dkt. D. James Kennedy alisema,

     Huu ni ukweli ulio muhimu zaidi. Katika historia ya saikolojia haijawahi julikana kwamba mtu angekusudia kuachilia maisha yake kwa jambo alilolijua ni uongo. Nilikuwa nashangaa kwa nini Mungu aliruhusu Mitume na Wakristo wa kwanza wapitie mateso kama yale, makubwa sana, mateso yasiyoaminika…tunaona uaminifu, tabia, mateso, na vifo vya hawa mashahidi, ambao wengi wao walitia muhuri ushuhuda wao kupitia damu yao…Paulo Little alisema, “Watu watakufa kwa kile wanachoamini kuwa ukweli…Hata hivyo, hawatakufa kwa kile wanachojua kuwa uongo” (D. James Kennedy, Ph.D., Kwa nini ninaamini, Wachapishaji wa Thomas Nelson, toleo la 2005, uk. 47).

Watu hawa walikufa kwa sababu walisema ya kwamba walishuhudia kufufuka kwa Kristo kutoka kwa wafu:

Petro – alipigwa mijeledi halafu akasulibiwa kichwa kikielekea chini.
  Andrea – Alisulibiwa kwa msalaba uliokuwa na umbo la X.
    Yakobo, mwana wa Zebedayo – alikatwa kichwa.
      Yohana – alitiwa birikani ya mafuta yanayochemka, halafu
      wakamhamishia kisiwani cha Patmo.
        Filipo – alipigwa mijeledi halafu akasulibiwa.
          Bartholomayo – alichunwa ngozi na kusulibiwa.
            Mathayo – alikatwa kichwa.
              Yakobo, nduguye Bwana – alitupwa kutoka juu ya hekalu,
              na halafu akapigwa hadi akafa.
                Thadayo – alichomwa na mishale hadi akafa.
                  Marko – alikokotwa chini hadi akafa.
                    Paulo – alikatwa kichwa.
                      Luka – alisulibiwa kwa mti wa mzeituni.
                        Tomaso – alichomwa na mikuki,
                          na akatupwa katika miali ya tanuru.
(Kitabu cha wafia dini cha New Foxe, Bridge-Logos Publishers, 1997, uk. 5-10;
Greg Laurie, Kwa nini ufufuo? Tyndale House Publishers, 2004, uk. 19-20).

Watu hawa walipitia mateso makali, na wakafa vifo vibaya, kwa sababu walisema kwamba Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. Watu hawafi kwa jambo ambalo hawajaliona! Watu hawa walimuona Kristo baada ya kufufuka kutoka kaburini! Hiyo ndiyo sababu mateso na kifo chenyewe havingeweza kuwasimamisha wasitangaze, “Kristo amefufuka kutoka kwa wafu!”

Petro alimwona pale ufuoni,
Wakala pamoja naye kado ya bahari;
Yesu alikuwa anasema, na midomo iliyokuwa imekufa,
“Petro, unanipenda?”
Aliyekuwa amekufa yu hai tena!
Aliyekuwa amekufa yu hai tena!
Alivunja, mfumbato wenye nguvu wa kifo –
Aliyekuwa amekufa yu hai tena!
   (“Yu hai tena” na Paulo Rader, 1878-1938).

Watu hawa walibadilishwa kutoka kwa waoga wasioamini na kuwa wafia dini wajasiri – kwa sababu walimwona Kristo baada ya kufufuka kutoka kaburini!

Tomaso alimwona pale chumbani,
Alimwita Bwana na Mungu,
Aliguza na vidole vyake alama
Zilizofanywa na misumari na upanga.
Aliyekuwa amekufa yu hai tena!
Aliyekuwa amekufa yu hai tena!
Alivunja, mfumbato wenye nguvu wa kifo –
Aliyekuwa amekufa yu hai tena!
   (Paulo Rader, ibid.).

Natamani kwamba makanisa yetu wangejifundisha tena kuimba wimbo huu ulio mkuu wa Paulo Rader! Ikiwa utaniandikia na kuuomba nitakutumia huu wimbo. Mwandikie Dkt. R. L. Hymers, Jr., S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015 – na uulize wimbo wa Paulo Rader “Yu Hai Tena.”

Tunaweza kuongeza ushahidi zaidi wa kufufuka kwa Kristo, lakini hilo alitakusadikisha. Watu wengine ambao walimwona Kristo baada ya kufufuka kutoka kwa wafu “walitia shaka” (Mathayo 28:17). Lazima muje kwa Kristo kwa imani. Kristo kabla hajachukua mwili alisema,

“Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” (Yeremia 29:13).

“Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki” (Warumi 10:10).

Nilikutana na Kristo aliyefufuka saa 10:30 asubuhi, Septemba 28, 1961 katika ukumbi wa Chuo cha Biola (sasa ni Chuo Kikuu) baada ya kusikiliza mahubiri yaliyohubiriwa na Dkt. Charles J. Woodbridge, aliyekiacha Chuo cha Fuller Theological Seminary mwaka wa 1957 kwa sababu walianza kuyakubali mambo nje ya Biblia (tazama Harold Lindsell, Ph.D., Vita vya Biblia, Zondervan Publishing House, toleo la 1978, uk. 111). Na wewe pia unaweza kumjua Kristo aliyefufuka – ikiwa unataka kumjua vizuri “Jitahidi kuingia katika mlango ulio mwembamba” (Luka 13:24). Unapokuja kwa Kristo dhambi zako zimelipiwa na kuoshwa kwa Damu Yake – na umezaliwa upya kupitia kufufuka kwake kutoka kwa wafu. Ni ombi langu kwamba utakuja kwa Kristo hivi karibuni! Amina.


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Jack Ngann:
“Katika Kristo Pekee” (na Keith Getty na Stuart Townend, 2001).


MWONGOZO WA

THIBITISHO TATU ZA KUFUFUKA KWA KRISTO

THREE PROOFS OF CHRIST’S RESURRECTION

na Dr. R. L. Hymers, Jr.

“Kwa maana mfalme anajua habari za mambo haya, nami naweza kusema naye kwa ujasiri, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua, kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni” (Mdo 26:26).

(Mdo 25:19; I Wakorintho 15:14)

I.   Kwanza, kaburi tupu, Mathayo 28:12-15; Yohana 20:19;
Mathayo 27:63-64, 65, 66.

II.  Pili, taarifa ya walioshuhudia, Yohana 20:19; Mdo. 1:3;
I Wakorintho 15:5-8.

III. Tatu, mateso ya Mitume, Mathayo 28:17;
Yeremia 29:13; Warumi 10:10; Luka 13:24.