Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




MAELEZO KUHUSU SIKU YETU YA KUFUNGA
ITAKAYOKUWA JUMANNE

NOTES ON OUR FAST-DAY ON TUESDAY
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyo hubiriwa Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana Jioni ya, Agosti 12, 2018
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Evening, August 12, 2018

“Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu. Akiba Ya Mbinguni” (Mathayo 6:17, 18).


Kumbuka kwamba Yesu hakusema,“Ikiwa utafunga.” Hapana, Alisema, “Utakapo funga.” Kufunga huonekana jamba la kigeni kwa watu wa ulimwengu leo. Wakati mwingine mama mwenye wasiwasi atafikiria utakufa kwa njaa ikiwa utamaliza siku bilka kula. Usimwambie mamako uongo. Mwambie tu hautakula hicho chakula.

Si kila mtu anastahili kufunga. Ikiwa una tatizo la kiafya unastahili kumuona daktari kabla ya kufunga. Katika kanisa letu, unaweza kumuona Dkt. Yudithi Cagan, ama Dkt. Kreighton L. Chan. Ama unaweza kuwapigia simu. Nambari ya simu ya Dkt. Yudithi Cagan ni (213)324-3231. Nambari ya simu ya Dkt. Chan ni (323)819-5153. Ikiwa una tatizo la kisukari au shinikizo la damu, ama tatizo lingine, hakikisha umempigia simu Dkt. Yudithi Cagan ama Dkt. Chan, ama uongee na mmoja wao baada ya ibada hii. Wakikuambia usifunge, Unaweza bado kuwa na muda zaidi wa maombi tutakapokuwa tumefunga siku ya Jumanne. Unaweza kuungana nasi katika maombi bila kufunga siku hiyo.

Jumanne, Agosti 14, tutakuwa na siku ya kufunga hapa kanisani kwetu. Haijakubidi kufunga. Hakuna mtu atakuwa akiangalia ikiwa umefunga. Ikiwa utafunga pamoja nasi itakuwa kwa hiari kabisa. Funga ikiwa unataka kufunga. Usifunge ikiwa hautaki.

Hii ndio mara ya kwanza tumekuwa na siku ya kufunga baada ya miezi kaadhaa. Nilikumbushwa kuhusu umuhimu wa kufunga na kuomba na Dkt. Elmer L. Towns, mwanzilishi mwenza wa Chuo Kikuu cha Liberty. Mawazo na maelezo nitakayodokeza katika ujumbe huu nimeyakusanya kutoka kwa kitabu cha Dkt. Towns kitwacho, Mwongozo wa anayeanza kufunga, Kimepigwa chapa na Bethany House Publishers, 2001. Ni kitabu kizuri. Ikiwa unahitaji nakala, unaweza kuagiza kimoja kutoka Amazon.com.

Kuna aina nyingi za kufunga katika kitabu cha Dkt. Towns. Lakini tutakuwa na siku moja ya kufunga, anayoiita “Saumu yaYom Kippur.” Hii ilikuwa siku moja ya kufunga ambayo Wayahundi waumini walihitajika kuizingatia (Walawi 16:29).

Leo, hawahitajiki kufunga – lakini tumeruhusiwa kufunga. Yesu alisema, “Mnapofunga” (Mathayo 6:16) kwa sababu kufunga ni nidhamu inayotusaidia kuimarisha tabia na imani.

Ikiwa haujawahi funga unaweza situka unapofikiria kwamba utamaliza siku bila kula chakula. Lakini kufunga hakutakuumiza kuliko vile unavyoumia unapojiweka katika nidhamu ya chakula bora ili kupunguza uzito. Kufunga kwa siku moja hakutamuumiza mtu “ALIYERUHUSIWA” na daktari – kama Dkt. Yudithi Cagan or Dkt. Chan.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

MAHUBIRI YETU YANAPATIKANA KATIKA RUKONO YAKO SASA.
INGIA KATIKA WWW.SERMONSFORTHEWORLD.COM.
BONYEZA KITUFE CHA KIJANI KILICHO NA NENO “APP”.
FUATA MAAGIZO YATAKAYOFUATA.

+ + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + + +

Siku moja ya “Saumu yaYom Kippur” ndio njia iliyobora kuzingatia utakapofunga siku ya Jumanne. Huhitajiki kufunga. Unafunga kwa hiari kama nidhamu ya kiroho. Usijali wengine watasema nini, kwa sababu kufunga kwako ni ahadi ya kibinafsi kati yako na Mungu. Kufunga kutakufanya uwe shujaa wa maombi wa Mungu.

Utakapofunga Jumanne tarajia pingamizi. Shetani atakupinga. Ikiwa utawaombea watu ili waokoke ama kuliombea kanisa lako, Shetani atakupinga. Kufunga si rahisi. Hivyo utakapoanza safari hii ya kufunga ifanye kwa maarifa kwa sababu inaweza kuwa ngumu. Lakini tuzo itakuwa ya thamani!

Siku moja ya kufunga ya Yom Kippur ilikuwa kutoka machweo hadi machweo katika Biblia. Ikiwa utafunga pamoja nasi kwa siku moja itabidi angalau ule kumbwe kabla ya machweo (kama saa mbili na nusu jioni). Ule ndizi ama bakuli ndogo ya nafaka. Siku inayofuata usile kifunguakinywa ama chakula cha mchana. Jua litakapotua Jumanne tutakuwa na chakula kwa ajili yako hapa kanisani. Unaweza kula kumbwe, kama ndizi nyingine, kabla haujakuja kanisani Jumanne saa moja jioni. Tutakuwa na uji na vipande vya mkate kwa ajili yako utakapofika hapa. Tutakuwa na maombi, na nafasi yako ya kushuhudia kuhusu siku yako ya kufunga na kuomba, na nitahubiri mahubiri mafupi.

UTAKAPOFUNGA NA KUOMBA JUMANNE, NI LAZIMA UWE NA KUSUDI. KUSUDI LA HII SIKU YA KUFUNGA NI KUMWOMBA MUNGU AUTUMIE MPANGO WETU WA JUMAMOSI KATIKA ULE MCHEZO WA WANAUME ILI KUWALETA WATU KANISANI. IKIWA MUNGU HATAUBARIKI ULE MCHEZO HAKUNA MTU ATAKAYEKUJA KANISANI, NA ILE MICHEZO ITAKUWA TU KAMA SHUGHULI ZINGINE ZA KAWAIDA, SEHEMU YA “MATENGENEZO” YA KANISA, KAMA SHUGHULI NYINGINE AMBAYO HAIZAI MATUNDA. TUTAKUWA NA SIKU NYINGINE YA KUFUNGA KUOMBEA SHUGHULI NYINGIE JIPYA AMBAYO WANAWAKE WATAKUWA NAYO SIKU CHACHE SIJAZO. LAKINI NAMUULIZA KILA MMOJA, WANAWAKE KWA WANAUME, WAFUNGE NA WAOMBE ILI MUNGU AITUMIE MICHEZO YA JUMAMOSI JIONI KUWALETA WATU WAPYA KANISANI KWETU. UNAWEZA OMBEA MAMBO MENGINE – LAKINI KUSUDI KUU LA MFUNGO HUU NI KUMWOMBA MUNGU KUITUMIA MICHEZO YA JUMAMOSI KUWALETA VIJANA WAPYA KANISANI KWETU. KUSUDI LAKO LA MAOMBI ULIELEKEZE KWA HILO – ILI MUNGU AWASAIDIE WANAUME KUWALETA WATU KATIKA ILE MICHEZO NA BAADAYE WALITEMBELEE KANISA LETU KATIKA IBADA ZA JUMAPILI. OMBA NA UFUNGE KWA KUSUDI HILO. TUNAHITAJI WANAWAKE WAFUNGE PAMOJA NASI PIA KWA KUSUDI HILI.

Kumbuka kuanza mfungo wako Jumatatu jioni kwa kula kumbwe kindogo, halafu usile kifunguakinywa na chakula cha mchana Jumanne. Halafu tena ule kumbwe kindogo inapokaribia jioni, halafu uje kanisani Jumanne saa moja jioni, na tutafungua pamoja kwa kunywa uji na vipande vya mikate.

“Mnapofunga”... Hii ni kumaanisha ya kwamba Yesu aliidhinisha kufunga. Wakristo wanastahili kufunga na kuomba ili kupokea nguvu na mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Dkt. Yohana R. Rice alisema, “Ninajua mfungo halisi...utaleta baraka ambazo Mungu anataka kutupatia.” Spurgeon alisema, “Tumepoteza baraka kuu katika kanisa la Wakristo kwa kupuuza kufunga.” Dkt. R. A. Torrey alisema, “Ikiwa tungeomba kwa nguvu, lazima tuombe na tufunge.” Mwinjilisti mashuhuri Yohana Wesley alisema, “Umetenga siku za kufunga na kuomba? Karibia kiti cha neema...na rehema zitashuka chini.” Mchungaji wangu Mchina, Dkt. Timotheo Lin alisema, “Ufahamu wetu wa kiroho mara nyingi unafunguliwa punde tunapoanza kufunga na kuomba...Nazungumza haya kutokana na uzoefu wangu binafsi.”

Nenda nyumbani na makala ya mahubiri haya usiku huu. Soma mahubiri haya kesho utakapokuwa ukijiandaa kuanza kufunga utakapokuwa ukila kumbwe. Hapa kuna mambo muhimu ya kukumbuka utakapofunga kuanzia Jumatatu usiku hadi Jumanne jioni:

1. Mfungo wako uwe siri (inavyowezekana). Usiende ukiwambia watu ya kwamba umefunga.

2. Kariri Isaya 58:6 wakati wa mfungo wa Jumanne.

“Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?” (Isaya 58:6).

3. Soma Mathayo 7:7-11 kwa makini mara kadhaa unapofunga Jumanne.

“Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango. “Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? Au akimwomba samaki atampa nyoka? Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? (Mathayo 7:7-11).

4. Ombea wanaume wetu ili wawalete vijana kadha katika mchezo wa vikapu Jumamosi, Agosti 18.

5. Unywe maji mengi, kama glasi moja baada ya kila masaa mawili. Unaweza pia kunywa kahawa au chai (bila maziwa au sukari) kama umezoea kunywa kila siku. Ukijisikia “hauna nguvu” unaweza kunywa soda baridi aina ya sprite ama seven-up (glasi moja au mbili). Usinywe vinywaji vya kuongeza nguvu!

6. Ukiwa na maswali kuhusu afya yako, kama shinikizo la damu na kisukari, zungumza na Dkt. Yudithi Cagan ama Dkt. Kreighton Chan kabla haujaanza kufunga. Nambari zao za simu zimepeyanwa mapema katika ujumbe huu.

7. Anza kufunga utakapokula kumbwe Jumatatu jioni. Tamatiza kufunga kwa kula kumbwe Jumanne jioni – halafu uje kanisani upate chakula saa moja Jumanne jioni.

8. Kumbuka kuyaelekeza maombi yako Jumanne kuwaombea wanaume wetu wafanikiwe kuwaleta watu katika mchezo wa mpira wa vikapu Jumamosi ijayo.

Unaweza kunipigia simu mimi, Dkt. Hymers, kupitia nambari hii (818)352-0452 wakati wowote ikiwa uko na tatizo ama swali ama unaweza kumpigia simu Bi. Hymers kupitia nambari hii (818)645-7356 na umwambie unanihitaji.

Nitakuwa nakuombea ili uwe na wakati wa kufana wa kuomba na kufunga! Jambo linguine moja: Ikiwa unafanya kazi ama uko shuleni siku ya Jumanne, ombea mahitaji haya kimoyomoyo mara kwa mara. Uwe na mahubiri haya Jumanne ili uweze kusoma mara kwa mara mambo haya manane muhimu (yaliyoandikwa hapo juu). Mungu awabariki nyote!

Dkt. R. L. Hymers, Jr.
Wafilipi 4:13

Tafadhali simama na uimbe wimbo nambari 4, “Nifundishe kuomba.”

Nifundishe kuomba, Bwana, nifundishe kuomba; Hiki ndicho kilio cha moyo wangu, siku baada ya siku;
Natamani kujua mapenzi Yako na njia Zako; Nifundishe kuomba, Bwana, nifundishe kuomba.

Nguvu katika maombi, Bwana, nguvu katika maombi, Hapa ‘duniani’ kuna dhambi na huzuni na mashaka;
Watu wamepotea, nafsi katika mashaka; Ee nipe nguvu, nguvu katika maombi!

Nifundishe kuomba, Bwana, nifundishe kuomba; Wewe ni kielelezo changu, siku baada ya siku;
Wewe ni mdhamini wangu, sasa na hata milele; Nifundishe kuomba, Bwana, nifundishe kuomba.
(“Nifundishe kuomba” na Albert S. Reitz, 1879-1966).


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Benjamini Kincaid Griffith:
“Nifundishe kuomba” (na Albert S. Reitz, 1879-1966).