Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




MASHAMBULIZI DHIDI YA MILANGO YA KUSIMU!

STORMING THE GATES OF HELL!
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana asubuhi ya, Julai 8, 2018
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angeles
Lord’s Day Morning, July 8, 2018


Tafadhali fungua katika Bibilia Mathayo 16:18, sehemu ya pili ya aya. Iko katika ukurasa 1021 katika Bibilia yenye mafunzo ya Scofield. Yesu alisema,

“na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda” (Mathayo 16:18b).

Mfafanusi R. C. H. Lenski alisema, “Maana halisi ni kwamba milango ya kusimu itaachilia jeshi [la mapepo] kulishambulia kanisa la Kristo, lakini kanisa halitapinduliwa” (Elezo la Lenski, kwa Mathayo 16:18b). Bila shaka hii inahusu kanisa la kweli, si kanisa lililokengeuka la siku za mwisho. Kanisa lililokengeuka tayari limejawa na roho za mapepo. Bibilia ilitabiri hili,

“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani” (I Timotheo 4:1).

Kazi ya Shetani na mapepo itawafanya wengi katika kanisa lisilo la kweli “kuacha imani” iliyowekwa katika neno lililopeyanwa na-Mungu katika Bibilia.

Matokeo ya mambo haya ni kanisa lisilo la kweli la “siku za mwisho” linaloelezewa katika II Timotheo 3:1-8, mahali ambapo kuna washirika wengi kanisani.

“wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao” (II Timotheo 3:4, 5).

Hivyo basi tunaona katika Bibila ya kwamba kuna kanisa aina mbili leo – kanisa la uongo, na kanisa la kweli. Yesu alitoa ahadi hii kwa kanisa la ukweli pekee,

“na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda” (Mathayo 16:18b).

Tumezungukwa na makanisa ya uongo katika Marekani siku ya leo. Makanisa ya uongo ni kama kanisa la Laodikea, ambalo katika maelezo ya Scofield linaelezewa kuwa katika “hatua ya mwisho ya mkengeuko.” Hapa kuna maelezo ya Yesu kuhusu mkengeuko wa Kilaodikea katika makanisa mengi leo:

“Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi” (Ufunuo 3:17).

“Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu” (Ufunuo 3:16).

Kutokana na kusikiliza mafundisho ya kipepo (I Timotheo 4:1) na wakiwa na aina ya inje tu ya Ukristo (II Timotheo 3:4, 5) mengi ya makanisa ya kiinjilisti katika siku hizi za mwisho yamekengeuka. Kama alivyonena Dkt. Yohana MacArthur waziwazi kwamba, washirika wa makanisa haya hawana ari, na ni “vuguvugu, wanafiki, wanaokiri kumjua Yesu, lakini si wa Yesu...hawa wanafiki waliojidanganya [wanachukiza] Kristo.” Ingawa Dkt. MacArthur amekosea kuhusu Damu ya Kristo, ako sahihi anapoeleza kwamba Wakristo wengi wa kiinjilisti ni “wanafiki waliojindanganya.”

Na hii ndio sababu makanisa ya kiinjilisti wanapoteza karibu vijana wote. Jonathani S. Dickerson ameandika kitabu kinachoitwa, Mwanguko Mkuu wa Kiinjilisti (Vitabu vya Baker). Alitoa takwimu za kweli. Leo ni asilimia 7 tu ya vijana wanaokiri kuwa Wakristo. Hesabu ya vijana wa Kiinjilisti bado kidogo itashuka kutoka asilimia 7 hadi karibu asilimia “4 tu ama chini – isipokuwa wanafunzi wapya waokolewe” (Dickerson, uk. 144).

Ni kwa nini kumekuwa na kushuka kwa idadi kubwa ya vijana kanisani leo? Sababu kuu ni kwamba wanaona washirika wengi kanisani kama “wanafiki waliojindanganya,” kama alivyosema Yohana MacArthur. Wanawaona washirika wazee kama wanaotapatapa, wadhaifu na bila uwezo wa kukabili ulimwengu wa dhambi unaowazunguka, hiyo ndiyo sababu! Mwanatheolojia Dkt. Daudi F. Wells ana huo mtazamo pia. Hiyo ndio sababu aliandika kile kitabu, Hakuna nafasi ya ukweli: ama Kilichotendeka kwa Theolojia ya Kiinjilisti? (Eerdmans, 1993). Mwanatheolojia mashuhuri Dkt. Carl F. H. Henry ana huo mtazamo pia. Alisema,

“Kizazi kisima kinakua bila habari ya wokofu [kusaliwa mara ya pili]. Wakatili wanachochea katika mavumbi ya ustaarabu uliopotoka na wananyatanyata katika kivuli cha kanisa lililo na ulemavu” (Mapambazuko ya Ustaarabu mkuu, Vitabu vya Crossway, uk. 15-17).

Kanisa lililo lemazwa.” Hivyo ndivyo Dkt. Carl F. H. Henry aliliita kanisa la kiinjilisti! “Kanisa lililo lemazwa.” Na mhubiri mashuhuri Dkt. Martyn Lloyd-Jones alizungumzia kuhusu “Mkengeuko hatari ambao kwa wingi umeonekana katika kanisa kwa miaka mia moja iliopita” (Ufufuo, Vitabu vya Crossway, uk. 57).

Tunapoteza karibu vijana wote katika makanisa. Tunashindwa kabisa “kuwaleta wanafunzi wapya.” Dkt. Wells alisema, “Kanisa la kiinjilisti limepoteza uasilia wake.” Makanisa ya kiinjilisti yana uororo, udhaifu, undani na ufinafsi – wanaogopa kuongea wazi ama kuwachochea watu kuwa wanafunzi wa kweli. Si ajabu vijana hawapendezwi!

Hatuko hapa kukufanya wewe kuwa mtu wa kiinjilisti aliyemdhaifu na mfinafsi. Tuko hapa kukufanya wewe kuwa mwanafunzi wa kweli wa Yesu Kristo! Hilo ndilo lengo letu kama kanisa. Lengo letu ni kuwaongoza vijana kufikia kilele chao katika Kristo. Tuko hapa kukuongoza kuwa mshindi wa medali ya dhahabu kwa ajili ya Yesu Kristo na Ufalme Wake! Vijana, waliochaguliwa, wako tayari kwa changamoto za Ukiristo wa Kiprotestanti.Wale ambao hawako tayari kwa Ukiristo wa Ukalvini ulio na nguvu watajiondoa! Kumbuka ya kwamba Yesu alisema, “Wengi wameitwa, lakini wachache wamechaguliwa.”

Huu si wakati wa kupunguza uijilisti. Usiku uliopita tulikuwa na chajio na halafu tukatazama sinema ya “Paulo, Mtume wa Kristo” hapa kanisani. “Paulo, Mtume wa Kristo” ilionyesha majaribu na taabu Wakristo wa karne ya kwanza walipitia ili kuwa wanafunzi wa kweli wa Kristo. Adhuhuri ya leo tutaenda nje kuwahubiria vijana wengine ili wawe wanafunzi wa kweli. Tutakuwa na wakati mzuri, tukimtii Kristo. Kristo alisema, “Nenda katika barabara na vichorochoro vya mji, na uwashurutishe watu kuingia ili nyumba yangu ijae.” Yesu Kristo alikufa katika msalaba wenye damu kutuokoa. Yesu Kristo alifufuka kimwili, nyama na mifupa, kutoka kwa wafu kutupatia uzima!

Najua Yesu Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. Najua hili kila siku, si wakati wa pasaka tu. Najua hili usiku ninapolala. Najua hili asubuhi, na mchana kutwa. “Hayuko hapa – Amefufuka kutoka kwa wafu!” Najua Kristo alifufuka kutoka kwa wafu kwa sababu Neno la Mungu linasema hivyo! Anakufikia kwako asubuhi ya leo kupitia midomo ya huyu mzee mkongwe. Anakujia. Anakwambia – “Ninaishi milele.” Na kwa sababu Kristo yu hai ninajua kile anaweza kufanya. Kwa sababu anaishi hata wewe unaweza kuishi pia. Kwa sababu anaishi milele, unaweza kuishi milele kupitia neema Yake. Hakuna mwisho wa mwanafunzi wa kweli wa Kristo. Njoo huende nasi katika kesho inayongaa ya uzima wa milele na Yesu. Hatakupungukia! Njoo, utuzaidie kulifanya hili kanisa kikosi cha askari jeshi, jeshi lenye nguvu la Kristo na Ufalme Wake!

Kasisi Yohana Cagan ana umri wa miaka 24. Yeye ni mwanafunzi wa Yesu. Yeye ni askari wa msalaba. Yeye ni mshindi wa nishani ya dhahabu katika Ufalme wa Yesu. Nimesoma mahubiri atakayohubiri 6:15 usiku huu! Ni mojawapo ya mahubiri yanayotia moyo ambayo nimewahi kusoma. Njoo na umruhusu Mchungaji Yohana akutie moyo kuungana naye kulifanya hili kanisa kuwa mnara wenye taa, na jeshi la askari linalopambana na vikosi vya mapepo ya Shetani!

Inukeni, watu wa Mungu! Umefaulu kwa mambo madogo;
Jitolee kwa moyo na nafsi na nguvu Kumtumikia Mfalme wa wafalme.

Inukeni, watu wa Mungu! Kanisa linawangoja,
Nguvu zake si sawa na jukumu lake; Inukeni, na mlifanye kuwa kuu!
   (“Inukeni, Enyi watu wa Mungu” na William P. Merrill, 1867-1954;
      ulibandilishwa na Mchungaji).

Ni nambari 1 katika karatasi yako ya nyimbo. Simama na huimbe huu wimbo!

Inukeni, watu wa Mungu! Umefaulu kwa mambo madogo;
Jitolee kwa moyo na nafsi na nguvu Kumtumikia Mfalme wa wafalme.

Inukeni, watu wa Mungu! Kanisa linawangoja,
Nguvu zake si sawa na jukumu lake; Inukeni, na mlifanye kuwa kuu!

Mnaweza kuketi.

Naam, tunaishi katika nyakati ambazo makanisa ya kiinjilisti yana udhaifu na mkengeuko sawa sawa na kanisa la Laodikea. Naam, wanapoteza karibu vijana wao wote. Naam, hawawezi kuwatia moyo vijana wenzao ili kuungana nao. Naam, wana uororo, ni walegefu na wasiopendeza. Naam, Nakumbuka jinsi walivyo “nizuia” nilipokuwa kijana kama wewe. Niliwaasi, na uasi uliokuwa na utakatifu, uasi kama ule wa Martin Luther. Wengine wamesahau matengenezo. Waacheni walale. Njooni mtuzaidie kuwa na matengenezo hapa kanisani kwetu! Matengenezo sasa! Matengenezo kesho! Matengenezo milele!

Tunaweza kuwa na kanisa kama la Filadelfia katikati ya mkengeuko wa Laodikea? Kwa kanisa la Filadelfia Kristo alisema,

“Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu” (Ufunuo 3:8).

Tunaweza kuwa na kanisa lililojaa vijana walio wanafunzi asili wa Kristo? Unaweza kusema ni mwendo uliopotezwa. Ni vingumu. Napenda kile mwandishi wa hotuba za Rais Patrick J. Buchanan alisema, “Mwendo uliopotezwa ndio pekee unaostahili kupiganiwa.” Njooni tena muwe na chajio pamoja nasi 6:15 usiku huu. Njooni tena usiku huu na umruhusu Mchungaji Yohana Cagan akutie moyo kujiunga nasi katika vita – kwa kuwa hatujapoteza katika hii vita. Inaweza kuonekana hivyo, lakini ushinde utapatikana bila shaka. Kristo alisema, “Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, na milango ya Kusimu haitaweza kulishind.” “Milango ya Kusimu haitaweza kulishinda.” Milango ya Kusimu ni milango ya kifo. Milango ya Kusima haitatuzuia kwa sababu Kristo aliye Bwana wetu amefufuka kutoka kwa wafu! Kwa sababu anaishi “milango ya Kusimu” haitaweza” kutushinda! Amina. Njooni tena usiku huu saa 6:15. Milango ya Kusimu haitatushinda!

Nafunga na maneno haya yaliyo na changamoto kutoka kwa Dkt. Francis A. Schaeffer. Dkt. Schaeffer alikuwa mwanatheolojia mashuhuri, na nabii wa kweli wa nyakati zetu. Alisema, “Kanisa la kiinjilisti limekuwa na udunia na limekosa uaminifu kwa Kristo aliyehai...Nawapa changamoto. Ninahimiza kuwe na Wakristo asili, na hasa vijana Wakristo asili, watakao simama na kupinga kwa upendo chochote kilicho kibaya na kinachoharibu katika kanisa, utamaduni wetu, na hali yetu” (Janga Kuu la Kiinjilisti, uk. 38, 151).

Simama na huimbe wimbo nambari 2. Ni wimbo wa Martin Luther wa matengenezo! Huimbe kwa sauti kubwa uwezavyo!

Mungu wetu ni ngome imara, Nguzo isiyoshindwa,
   Yeye ni msaada wetu, katikati ya gharika ya maovu yaliyo kama desturi.
Kwa sababu adui wetu wa kitambo utafuta kutudhuru;
   Ujanja wake na nguvu zake ni kuu, Na akiwa na silaha za chuki,
Duniani hapana wa kutoshana naye.

Na ingawa dunia hii, iliyojawa na mapepo, itatisha kutuangamiza,
   Hatutaogopa, kwa sababu Mungu amekusudia ukweli wake kufanikiwa kutupitia.
Mkuu wa giza anatisha – Hatutetemeshi;
   Tutastahimili ghadhabu yake, Tazama! kuharibiwa kwake ni hakika,
Neno moja ndogo tu litamwangusha.

Neno hilo lililo juu ya nguvu zote za dunia – Hakuna shukrani kwao – inayodumu;
   Roho na karama ni zetu Kupitia Yeye aliye upande wetu.
Acha mali na jamaa, Maisha haya ya kufa pia;
   Wanaweza kuua mwili: Ukweli wa Mungu unadumu bado,
Ufalme Wake ni wa milele.
    (“Mungu wetu ni ngome imara” na Martin Luther, 1483-1546).

Mchungaji Yohana, tafadhali tuongoze kwa maombi na ushukuru kwa chakula.


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Benjamini Kincaid Griffith:
“Mungu wetu ni ngome imara” (na Martin Luther, 1483-1546).