Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




“NJIA YA NEEMA” NA GEORGE WHITEFIELD,
IMEFUPISHWA NA KUTOLEWA KWA KISWAHILI CHA KISASA

“THE METHOD OF GRACE” BY GEORGE WHITEFIELD,
CONDENSED AND ADAPTED TO MODERN ENGLISH
(Swahili)

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

Mahubiri yaliyohubiriwa na Bw. John Samuel Cagan
katika Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana njioni ya, Januari 8, 2017

“Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.” (Yeremia 6:14).


Utangulizi: George Whitefield alizaliwa kule Gloucester, Uingereza mwaka wa 1714. Alikuwa mwana wa kiume wa mtu aliyemiliki baa. Katika mazingira haya alikuwa na ushawishi mchache wa Ukiristo akiwa mtoto, lakini alikuwa na uwezo ambao haukuwa wa kawaida akiwa shuleni. Alisomea Chuo Kikuu cha Oxford ambapo alifanya urafiki na John na Charles Wesley na akawa mmoja wa kikundi chao cha maombi na kusoma Bibilia.

Alipokuwa mwanafunzi pale Oxford alipokea uongofu. Muda mfupi baadaye aliwekwa wakfu na Kanisa la Uingereza. Mahubiri yake ya umuhimu wa kuzaliwa upya yalisababisha makanisa mengi kumufungia milango, kwa sababu Wachungaji wa kimwili waliogopa kwamba mahubiri yake ya umuhimu wa kuzaliwa upya yangewakasirisha watu wa parokia. Hivyo, alitupwa nje ya makanisa, kuhubiri katika maeneo wazi, na hii ikamfanya kuwa mashuhuri.

Whitefield alisafiri Marekani mwaka wa 1738 na akaanzisha kituo cha mayatima. Baadaye alisafiri katika majimbo ya koloni za Marekani na Uingereza akihubiri na kuchangisha pesa kufadhili kituo cha mayatima. Alihubiri Uispania, Uholanzi, Ujerumani, Ufaranza, Uingereza, Wales, na Uskoti, na alisafiri mara kumi na tatu kupitia Atlantiki kuhubiri Marekani.

Alikuwa rafiki wa karibu na Benjamin Franklin, Jonathan Edwards na John Wesley, na ndiye aliyemshawishi Wesley kuhubiri katika maeneo wazi, kama alivyofanya. Benjamin Franklin alikisia kwamba mara moja Whitefield aliwasungumzia watu elfu thelathini. Mikutano yake ya nje mara nyingi ilihudhuriwa na watu waliozidi 25,000. Mara moja alihubiri karibu na Glasgow, Uskoti kwa zaidi ya watu 100,000 katika kusanyiko moja – katika siku ambazo hakukuwa na vipasha sauti! Watu elfu kumi walikiri kupokea uongofu katika ule mkutano.

Anachukuliwa na Wanahistoria wengi kuwa Mwinjilisti mkuu wa wakati wote aliyezungumza lugha ya Kiingereza. Ingawa Billy Graham amewazungumzia watu wengi akiwezeshwa na vipasha sauti vya elektroniki, ushawishi wa Whitefield kwa tamaduni bila shaka ulikua mkubwa.

Whitefield aliongoza katika Mwamko mkuu wa kwaza, ufufuo wa kina uliobadilisha tabia ya Amerika katikati ya karne ya kumi na nane. Majimbo katika nchi yetu yaliwashwa moto wa ufufuo alipohubiri. Kilele cha ufufuo huu kilikuja 1740 katika kipindi cha wiki sita Whitefield alipozuru New England. Kwa siku arobaini na tano tu alihubiri mahubiri zaidi ya mia moja sabini na tano kwa makumi ya maelfu ya watu, Na kuacha eneo hilo likiwa na msisimko wa kiroho, ni mojawapo ya nyakati muhimu katika Ukiristo wa Amerika..

Kufikia kifo chake alikuwa amependwa na kuangaziwa na ulimwengu wote ulio zungumza lugha ya Kiingereza. Alihusika katika kuanzisha Chuo Kikuu cha princeton, Chuo cha Dartmouth, na Chuo Kikuu cha Pennsylvania. Aliaga muda mfupi baada ya kuhubiri kule Newburyport, Massachusetts, mwaka wa 1770, miaka sita kabla ya Mapinduzi ya Amerika. George Washington alikuwa baba wa taifa letu, lakini George Whitefield ndiye alikuwa babu wa taifa hili.

Mahubiri yafuatayo ya Whitefield yametolewa kwa Kiingereza cha kisasa. Ni mahubiri yake halisi, lakini nimeyarekebisha maneno ili mahubiri haya yaeleweke wakati huu wetu.

“Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani” (Yeremia 6:14).

Mahubiri: Baraka ile kuu kabisa Mungu anaweza kulipatia taifa ni wahubiri wazuri na waaminifu. Lakini laana ile kuu kabisa Mungu anaweza tuma kwa taifa lolote ni kukubali makanisa yaongozwe na wahubiri waliopotea ambao wanajishugulisha tu na kujichumia pesa. Lakini katika kila wakati kumekuwa na wahubiri wa uongo ambao walihubiri mahubiri yenye kupendeza. Kuna wahubiri wengi wa namna hii wanao potosha na kuigeuza Bibilia kuwandanganya watu.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati wa Yeremia. Na Yeremia aliongea kinyume nao kwa utiifu uaminifu kwa Mungu. Alifungua kinywa chake na kuhubiri kinyume na hawa wahubiri wa kimwili. Ukisoma kitabu chake, utaona ya kwamba hakuna yeyote aliyewahi kuzungumza zaidi kinyume na wahubiri wa uongo kuliko Yeremia. Alizungumza kwa ukali kinyume nao katika sura iliyo na somo letu.

“Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani” (Yeremia 6:14).

Yeremia alisema wanahubiri tu kwa sababu ya pesa.Katika mstari wa kumi na tatu, Yeremia alisema,

“Kwa maana, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa miongoni mwao, kila mmoja ni mtamanifu; na, tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu” (Yeremia 6:13).

Wao ni wenye tamaa na wanahubiri kwa uongo.

Katika somo letu, Yeremia anaonyesha mojawapo ya njia wanayotumia kuhubiri uongo. Nabii anaonyesha njia ndanganyifu walizotumia kuhusika na nafsi zilizopotea:

“Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani” (Yeremia 6:14).

Mungu alimwambia Yeremia awaonye watu kuhusu vita vilivyokuwa vinakuja. Mungu alitaka Yeremia awaambie nyumba zao zingeharibiwa – ya kwamba vita vinakuja (Ona Yeremia 6:11-12).

Yeremia alipeyana ujumbe ulioguruma kama radi. Ujumbe huu ulistahili kuwatia hofu watu wengi na kuwaleta katika hali ya toba. Lakini manabii wa mwili na makuhani walizunguka wakiwapa watu faraja ya uongo. Walisema Yeremia alikuwa na itikadi za kiunyama. Walisema hakungekuwa na vita. Waliwambia watu kutakuwa na amani, wakati Yeremia alikuwa amesema hakungekuwa na amani.

“Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani” (Yeremia 6:14).

Maneno ya maandiko haya kimsingi yanazungumzia amani ya nje. Lakini pia yanahusu nafsi. Naamini pia yanahusu wahubiri wa uongo wanaowambia watu ni wazuri kabisa, hata ingawa hawajazaliwa mara ya pili. Watu wasioongoka upenda mahubiri ya namna hii. Moyo wa mwanadamu una uovu na undanganyifu. Mungu hujua jinsi usivyoaminika moyo wa mwanadamu.

Wengi wenu wanasema wako na amani na Mungu, wakati ambapo hakuna amani! Wengi wenu mnafikiria ninyi ni Wakristo, lakini hapana. Shetani ndiye amewapa Amani ya uongo. Mungu hakuwapa hii “amani.” Si amani inayopita ufahamu wa mwanadamu. Amani ulionayo ni ya uongo.

Ni muhimu kwako kujua kama una amani halisi na Mungu au la. Kila mtu anataka amani. Amani ni Baraka kuu. Hivyo inabidi nikwambie jinsi ya kupata Amani halisi na Mungu. Ni lazima niwe huru kutokana na damu yako. Ni lazima nikutangazie ushauri kamili wa Mungu. Kutokana na maneno ya maandiko, nitajaribu kukuonyesha kitakachotokea kwako, na kinachohitajika kubadilika ndani yako ili uwe na amani ya kweli na Mungu.

I. Kwanza, kabla ya kuwa na Amani na Mungu, ni lazima uwezeshwe kuona, kuhisi, kulia, na kuhuzunika kuhusu dhambi zako ulizo tenda kinyume na sheria ya Mungu.

Bibilia inasema, “roho ile itendayo dhambi itakufa.” (Ezekieli 18:4). Kila mtu amelaaniwa ambaye hatendi maneno yote yaliyo andikwa katika sheria ya Mungu.

Si lazima tu ufanye mambo fulani, lakini lazima utimize mabo yote au utakuwa umelaaniwa:

“maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye” (Wagalatia 3:10).

Kuvunja sheria yeyote ya Mungu, ikiwa ni kwa mawazo, au kwa maneno, au kwa matendo, inakufanya ustahili adhabu ya milele, kulingana na sheria ya Mungu. Na ikiwa wazo moja ovu, ikiwa neno moja ovu, ikiwa tendo moja ovu ustahili uharibifu wa milele, unaweza kuepuka Jahanamu aji? Kabla ya kuwa na amani ya kweli katika moyo wako, ni lazima uwezeshwe kuona ni jambo la hatari kutenda dhambi kinyume na sheria ya Mungu.

Chunguza moyo wako. Na hebu nikuulize – umewahi kuwa na wakati ambapo ulikumbuka dhambi zako na ikawa na uchungu kwako? Umewahi kuwa na wakati ambapo ulihisi mzigo wa dhambi zako haubebeki? Uliwahi kuona ya kwamba gadhabu ya Mungu hasa inaweza kukuangukia wewe, kwa sababu ya hali yako ya kukiuka sheria zake? Umewahi kuhisi unajuta ndani mwako kwa sababu ya dhambi zako? Ungeweza kusema, “Dhambi zangu ni nzito sana kwangu siwezi kusibeba?” Umewahi kuhisi jambo kama hili? Ikiwa hapana, usijiite Mkristo! Unaweza kusema uko na amani, lakini hakuna amani halisi kwako. Na Bwana aweze kukuamusha! Na Bwana aweze kukuokoa!

II. Pili, kabla ya kuwa na amani na Mungu, lazima uhukumike kwa kina; lazima ushawishike kuhusu hali yako halisi ya dhambi, na upotovu wa nafsi yako.

Lazima ushawishike kuhusu dhambi zako halisi. Ni lazima uwezeshwe kutetemeka juu ya dhambi zako. Lakini hali ya kuhukumika lazima iwe ya kina zaidi ya hiyo. Lazima uhukumike hasa kwa kuvunja sheria ya Mungu. Zaidi ya hiyo, ni lazima uhisi dhambi zako za asili, zinazozaliwa na moyo wako, ambazo zitakupeleka Jahanamu.

Watu wengu ambao ujifikiria ni werevu husema kwamba hakuna dhambi za asili. Wanafikiria ya kwamba Mungu si mwenye haki kuwapeleka Jahanamu kwa sababu ya dhambi walizorithi kutoka kwa Adamu. Wanasema hawakusaliwa katika dhambi. Wanasema hauhitaji kusaliwa mara ya pili.Lakini angalia ulimwengu unaokuzunguka. Je!ni paradiso Mungu aliyowaahidi wanadamu? La! Kila kitu katika ulimwengu kiko nje ya utaratibu! Hii ni kwa sababu kuna kitu kilichokasoro katika jamii ya binadamu. Ni dhambi ya asili ambayo imeharibu ulimwengu.

Haijalishi utalikataa hili kwa nguvu, Wakati utakapoamka, utaona ya kwamba dhambi ilyo katika maisha yako utoka kwa moyo wako uliopungukiwa – moyo uliotiwa sumu na dhambi ya asili.

Wakati mtu asiyeongoka anapata mwamko mara ya kwanza, anaanza kushangaa, “Nikawaje mwovu hivi?” Kisha Roho wa Mungu umuonyesha ya kwamba hana chochote kizuri katika hali yake ya asili. Basi yeye huona ya kwamba yeye ni mwenye dhambi kabisa. Halafu yule mtu hatimaye anaona ya kwamba Mungu ako na haki ya kumuangamiza. Anaona ya kwamba ametiwa sumu na uasi katika hali yake ya asili na kwamba ingekuwa haki kwa Mungu kumuangamiza, ata ingawa akutenda dhambi ata moja ya nje katika maisha yake yote.

Umewahi kupitia hili? Umewahi kuhisi hivi – ya kwamba ingekuwa sawa na ingekuwa haki kwa Mungu kukuadhibu ? Umewahi kubali ya kwamba kulingana na asilia yako wewe ni mtoto wa ghadhabu? (Waefeso 2:3).

Kama umewahi kuzaliwa mara ya pili, ungehisi hivi. Na kama haujawahi hisi uzito wa dhambi ya asili, usijiite Mkristo! Dhambi ya asili ndiyo mzigo mkubwa kwa mwongofu wa kweli. Mtu aliyezaliwa mara ya pili kwa kweli uhuzunishwa na dhambi zake za asili na asilia yake iliotiwa sumu. Mtu aliyeongoka kwa kweli ulia, “ Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?, hali hii ya dhambi inayokaa moyoni mwangu?” (ona.Warumi 7:24). Hili ndilo linalomsumbua zaidi mtu aliye na mwamko – moyo wake wa ndani wa dhambi. Kama haujawahi fahamu hali hii ya dhambi za ndani katika asilia yako, hakuna njia yeyote ya kupata amani ya kweli katika moyo wako.

III. Tatu, kabla ya kuwa na amani ya kweli na Mungu, si lazima tu usumbuliwe na dhambi zilizo katika maisha yako, na dhambi katika asilia yako, lakini pia kwa dhambi zinazohusiana na maamuzi yako bora, majukumu unayotenda, na hii-inayoitwa “Maisha ya Ukristo.”

Rafiki yangu, ni nini iliyo katika dini yako itakayokufanya ukubalike na Mungu? Wewe si mwenye haki na haujaongoka kulingana na asilia yako. Unastahili kuadhibiwa Jahanamu mara kumi kwa sababu ya dhambi zako. Ni wema gani itakayokutendea imani yako kwa dini yako? Hauwezi kuyatenda matendo mema bila kuwa umeongoka.

“Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu” (Warumi 8:8).

Ni vingumu kwa mtu asiyeongoka kufanya jambo lolote kwa utukufu wa Mungu.

Hata baada ya kuongoka, bado tunafanywa upya kwa sehemu. Dhambi ya ndani uendelea ndani yetu. Bado kuna mchanganyiko wa ubovu katika kila moja ya wajibu wetu. Kwa hiyo, baada yetu kuongoka, ikiwa Yesu Kristo angetukubali kulingana na kazi zetu “zuri”, kazi zetu zingetuangamiza. Hatuwezi hata kuomba pasipo na dhambi katika yale maombi, kama uchoyo, uvivu, maadili yasio kamilifu ya namna fulani. Sijui unafikiri nini, lakini siwezi kuomba bila kutenda dhambi. Siwezi kukuhubiria bila kutenda dhambi. Siwezi fanya jambo lolote bila dhambi. Toba yangu inahitaji ni itubu, na machozi yangu yaoshwe kwa damu ya thamana ya Mkombozi wangu,Yesu Kristo!

Maazimio yetu mazuri, kazi zetu zuri, dini zetu zuri, maamuzi yetu mazuri, ni dhambi tu nyingi. Kazi zetu za dini zimejaa dhambi. Kabla ya kuwa na amani moyoni mwako si lazima tu uhisi vibaya kwa sababu ya dhambi zako za asili na za kutenda, lakini ni lazima uchoshwe na haki yako wewe mwenyewe, kazi na udini. Lazima kuwe na kuhukumika kwa kina kabla ya kuondolewa kutoka kwa haki ya kibinafsi. Kama haukuhisi hivyo hauna haki yako binafsi, hauwezi kuokolewa na Yesu Kristo. Bado wewe haujaongoka.

Mtu anaweza kusema, “Sawa, Naamini haya yote.” Lakini kuna tofauti kubwa kati ya "kuamini" na "kuhisi." Umewahi hisi uhitaji wa Kristo? Umewahi hisi kwamba ulimuhitaji Kristo kwa sababu hauna uzuri wako mwenyewe? Na unaweza sasa kusema, "Bwana, unaweza kuniadhibu kwa kazi bora za dini ningeweza kufanya." Kama haujaletwa nje yako namna hii, hakuwezi kuwa na amani ya kweli na Mungu.

IV. Nne, kabla ya kuwa na amani na Mungu, kuna dhambi fulani moja ambayo ni lazima iwe inakusumbua. Na bado naogopa wachache wenu wataifikiria. Ndiyo dhambi iliyo na laana zaidi katika ulimwengu, na bado ulimwengu hauichukui kama dhambi. Unauliza, “Dhambi hiyo ni gani?” Ndiyo dhambi ambayo wengi wenu hawafikiri wana hatia kuihusu– na hiyo ni dhambi ya kutoamini.

Kabla ya kuwa na amani, ni lazima usumbuliwe na kutokuamini kwa moyo wako, kwamba wewe kwa hakika haujamwamini Bwana Yesu Kristo.

Nausihi moyo wako. Naogopa ya kwamba hauna imani zaidi katika Yesu Kristo kuliko Shetani mwenyewe. Nafikiri Shetani anaamini mengi katika Bibilia kukuliko wewe. Anaamini uungu wa Yesu Kristo. Anaamini na kutetemeka. Anatetemeka kuliko maelfu wanaojiita Wakrist leo.

Unafikiri unaamini kwa sababu unaamini Bibilia, ama kwa sababu uenda kanisani. Unaweza kuyafanya haya yote bila imani ya kweli katika Kristo. Kuamini tu kulikuwa na mtu kama Yesu hakutakufanya wema wowote, zaidi ya kule kuamini kulikuwa na mtu kama Kaisari au Aleksanda Mashuhuri. Bibilia ni neno la Mungu. Tunashukuru kwa sababu ya Bibilia. Lakini unaweza kuiamini, na bado husimwamini Bwana Yesu Kristo.

Nikikuuliza yapata miaka mingapi tangu ulipo mwamini Yesu Kristo, wengi wenu wangeniambia ya kwamba mmemwamini kila wakati. Haungenipa thibitisho zaidi ya kwamba bado haujamwamini Yesu Kristo. Wale wanaomwamini kwa kweli Kristo wanajua ya kwamba kulikuwa na wakati hawakumwamini.

Ni lazima niongee zaidi kuhusu hili, kwa sababu hii ni dhana ndanganyifu zaidi. Na imewachukua wengi – wakifikiria ya kwamba tayari wameamini. Mtu mmoja alisema ya kwamba aliorodhesha dhambi zake zote chini ya Amri kumi, halafu akaenda kwa Mchungaji na kumuuliza ni kwa nini hakuwa na amani. Yule muhuduma akaiangalia ile orodha na akasema, “Nenda! Sipati neno hata moja kuhusu dhambi ya kutoamini katika orodha yako.” Ni kazi ya Roho Mtakatifu wa Mungu kukushawishi kuhusu kutoamini kwako – kwamba hauna imani.Yesu Kristo alisema hivi kumhusu Roho Mtakatifu:

“Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi---ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi” (Yohana 16:8-9).

Sasa, rafiki zangu, Mungu aliwahi kukuonyesha kwamba haukuwa na imani halisi katika yesu? Uliwahi huzunika kwa majonzi juu ya moyo wako mgumu wa kutoamini? Uliwahi omba, “Bwana, nisaidie niweze kumwamini Kristo?” Mungu aliwahi kukusadikisha kuhusu hali yako ya kutokuwa na uwezo wa kuja kwa Kristo, na kukufanya upashe sauti ukiomba uwe na imani katika Kristo? Ikiwa hapana, hautaipata amani katika moyo wako. Mungu akuamshe, na akupe amani ya kweli kupitia imani kwa Yesu, kabla haujakufa na kukosa nafasi nyingine.

V. Tano, kabla ya kuwa na amani na Mungu, ni lazima uamini kikamilifu haki ya Kristo.

Si lazima tu usadiki dhambi zako za kutenda na za asili, dhambi za haki yako mwenyewe, na dhambi za kutoamini kwako, lakini ni lazima uwezeshwe kuamini haki iliyotimilifu ya Yesu Kristo. Lazima uishikilie haki ya Kristo. Halafu utakuwa na amani. Yesu alisema:

“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28).

Mstari huu unatia moyo wote wanaosumbuka na kulemewa, lakini si kwa mwingine yeyote. Bado ahadi ya pumziko imeahidiwa kwa wale wanaomwendea na kumwamini Yesu Kristo. Kabla ya kuwa na amani na Mungu ni lazima huesabiwe haki kwa imani katika Bwana wetu Yesu Christo. Lazima uwe na Kristo Mwenyewe, ili haki Yake ifanyike haki yako.

Rafika zangu wapendwa, umewahi kuolewa na Kristo? Je! Yesu Kristo alijipeyana kwako? Je! uliwahikuja kwa Kristo kwa imani iliyohai? Ninamwomba Mungu kwamba Yesu aje ainene amani juu yako. Ni lazima upitie haya mambo ili uzaliwe mara ya pili.

Sasa ninaongea kuhusu mambo yasiyoonekana ya dunia nyingine, ya Ukristo uliyo ndani, ya kazi ya Mungu katika moyo wa mwenye dhambi. Sasa ninayazungumzia mambo yaliyo na umuhimu mkubwa kwako. Ni lazima uhusike sana na hili. Nafsi yako inahusika kwa hili jambo. Wokovu wako wa milele unafungamana na hili.

Unaweza kuhisi amani pasipo Kristo. Shetani amekufanya ulale na akakupa usalama wa uongo. Atajaribu kukudumisha katika usingizi hadi akupeleke Jahanamu. Pale utaamka, Lakini utakuwa mwamko wa kuogofya unapojipata katika ndimi za moto mahali ambapo utakuwa umeshelewa kuokolewa. Kule Jahanamu utaitana milele yote ukiomba tone la maji ili kubaridisha ulimi wako, na hakuna maji utakayopewa.

Na usipate pumziko katika moyo wako hadi upate pumziko katika Yesu Kristo! Kusudi langu ni kuwaleta wenye dhambi waliopotea kwa Mwokozi. Ni ombi langu Mungu akulete kwa Yesu. Na Roho Mtakatifu akushawishi kwamba wewe ni mwenye dhambi, na akugeuze kutoka kwa njia zako bovu na akulete kwa Yesu Kristo. Amina.


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Maombi kabla ya Mahubiri: Bw. Noah Song.
Wimbo ulioimbwa kabla ya Mahubiri Bw. Benjamin Kincaid Griffith:
     “Ee Bwana, Mimi ni mpotovu kiasi gani” (John Newton, 1725-1807).


MWONGOZO WA

“NJIA YA NEEMA” NA GEORGE WHITEFIELD,
IMEFUPISHWA NA KUTOLEWA KWA KISWAHILI CHA KISASA

“THE METHOD OF GRACE” BY GEORGE WHITEFIELD,
CONDENSED AND ADAPTED TO MODERN ENGLISH

Mahubiri haya yameandikwa na Dkt. R. L. Hymers, Jr.
na kuhubiriwa na Bwana. John Samuel Cagan

“Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani” (Yeremia 6:14).

(Yeremia 6:13)

I.    Kwanza, kabla ya kuwa na amani na Mungu, ni lazima uwezeshwe kuona, kuhisi, kulia, na kuhuzunika kuhusu dhambi zako ulizo tenda kinyume na sheria ya Mungu. Ezekieli 18:4; Wagalatia 3:10.

II.   Pili, kabla ya kuwa na amani na Mungu, lazima uhukumike kwa kina; lazima ushawishike kuhusu hali yako halisi ya dhambi, na upotovu wote wa nafsi yako, Waefeso 2:3; Warumi 7:24.

III. Tatu, kabla ya kuwa na amani na Mungu, si lazima tu usumbuliwe na dhambi katika maisha yako, na dhambi katika asilia yako, lakini pia kwa dhambi zinazohusiana na mahamuzi yako bora, majukumu, na hii-inayoitwa “maisha ya Ukristo,” Warumi 8:8.

IV. Nne, kabla ya kuwa na amani na Mungu, ni lazima usumbuke kuhusiana na dhambi hii laanifu ya kutomwamini Yesu, Yohana 16:8,9.

V.  Tano, kabla ya kuwa na amani na Mungu, ni lazima uamini kikamilifu haki ya Kristo, Mathayo 11:28.