Print Sermon

Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.

Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.

Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.




YESU KRISTO MWENYEWE

JESUS CHRIST HIMSELF

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.
(Swahili)

Mahubiri yaliyohubiriwa Baptist Tabernacle kule Los Angeles
Siku ya Bwana, Asubuhi ya, Aprili 12, 2015
A sermon preached at the Baptist Tabernacle of Los Angelse
Lord’s Day Morning, April 12, 2015


Hii ni siku kuu kwa mke wangu Ileana na mimi. Sisi wawili tunasherehekea siku yetu ya kusaliwa leo. Siku hii, Aprili 12, ndiyo siku ya sabini na nne ya kuzaliwa kwangu. Leo pia ni siku ya maadhimisho ya miaka hamsini na saba ya wito wangu katika huduma tangu mwaka wa 1958. Lakini, zaidi ya hayo, hii ni siku kuu kwa kanisa letu. Miaka arubaini iliopita nilianzisha kanisa hili na vijana kama sita au saba katika chumba nilichoishi, katika makutano ya Westwood na Wilshire Boulevard, hatua chache kutoka UCLA, chuo mashuhuri magharibi mwa Los Angeles. Ni watu wawili tu waliosalia hapa, Bw. Yohana Cook na mimi. Kwa neema ya Mungu, Yohana na mimi tuko hapa asubuhi ya leo – baada ya miaka arubaini. Na Yesu Kristo apokee sifa!

Kanisa hili limepitia miaka arubaini ya majaribu. Kama vile wana wa Israeli walikaa jangwani miaka arubaini, hivyo kanisa hili limepitia shida nyingi, taabu nyingi, na mateso mengi. Nitazungumza mengi kuhusu haya usiku huu. Lakini tuko hata leo, kanisa kuu linalohubiri Injili katikati mwa mji wa Los Angeles. Na tunajua ya kwamba katika mateso yote, Mungu amekuwa pamoja nasi na ametupa ushindi mkuu tunaosherehekea leo, tunapoadhimisha miaka arubaini ya kanisa letu! Na Yesu Kristo apokee sifa!

Mchungaji Roger Hoffman alihubiri katika mkutano wetu wa maombi jana usiku. Atahubiri tena leo usiku katika sherehe za maadhimisho yetu. Lakini Mchungaji Hoffman hakuitikia nilipomuuliza ahubiri asubuhi hii. alisema, “Dkt. Hymers, nataka kukusikiza ukihubiri Jumapili asubuhi.” Halafu, nilipokuwa nikiomba kuhusu jambo nitakalolisema, niliongozwa kurudia mahubiri niliyohubiri katika kanisa lingine la Kibaptisti Agosti, 2010. Tafadhali fungua pamoja nami kitabu cha Waefeso, sura ya pili. Iko katika ukurasa wa 1251 katika Bibilia ya kujifunza ya Scofield. Simama ninaposoma Waefeso 2:19, 20.

“Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.” (Waefeso 2:19, 20).

Mnaweza kuketi.

Hapa katika andiko hili Mtume Paulo anatuambia ya kwamba kanisa ni watu wa nyumba ya Mungu. Halafu anatuambia ya kwamba kanisa limejengwa katika misingi ya mitume na manabii, lakini Yesu Kristo Mwenyewe ndiye “jiwe kuu la pembeni.” Dkt. J. Vernon McGee alisema hili linamaanisha ya kwamba “Kristo ndiye mwamba ambapo kanisa limejengwa” (Kupitia Bibilia, Sehemu V, Thomas Nelson, k. 241; maelezo ya Waefeso 2:20). Dkt. A. T. Robertson alisema, “akrogōniais...ni jiwe kuu la msingi” (Picha za maneno, Broadman, 1931; maelezo ya Waefeso 2:20). Yesu Kristo Mwenyewe ndiye msingi wa kazi zetu zote, na maisha yetu yote. “Yesu Kristo Mwenyewe” ndiye msingi wa kanisa. Nayatumia maneno haya yaliyo mwisho wa Waefeso 2:20 kama somo letu asubuhi hii.

“Kristo Yesu mwenyewe” (Waefeso 2:20).

Yesu Kristo Mwenyewe ndiye mada ya mahubiri haya. Imani ya Kikristo haina jambo lililo la kupendeza kuliko Yesu Kristo Mwenyewe. Hakujawahi kuwa wala hakutawahi kuwa na yeyote mwingine kama Yesu. Yeye ni wa kipekee kabisa katika historia ya mwanadamu. Yesu Kristo Mwenyewe ni Mungu-mwanadamu. Yesu Kristo Mwenyewe alishuka kutoka mbinguni na akaishi pamoja na watu. Yesu Kristo Mwenyewe aliteseka, alimwaga damu na akafa kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu Kristo Mwenyewe alifufuka kimwili kutoka kwa wafu ili tuhesabiwe haki. Yesu Kristo Mwenyewe alipaa tena mbinguni na amekaa mkono wa kuume wa Mungu akituombea. Na Yesu Kristo Mwenyewe atakuja tena kuanzisha Ufalme Wake hapa duniani kwa miaka elfu moja. Huyo ni Yesu Kristo Mwenyewe! Simama na uimbe kibwagizo hiki!

Yesu pekee, acha nimuone,
   Yesu pekee, hakuna mwingine ila Yeye,
Halafu wimbo wangu utakuwa milele –
   Yesu! Yesu pekee!
(“Yesu pekee, Acha nimuone” na Dkt. Oswald J. Smith, 1889-1986).

Mnaweza kuketi.

Mada ya ni Yesu Kristo Mwenyewe ni ya undani kabisa, na ni pana, na ya muhimu kabisa kiasi kwamba hatuwezi kuieleza yote kwa ujumbe mmoja. Tunaweza tu kuguzia maneno muhimu machache asubuhi hii kuhusu Yesu Kristo Mwenyewe.

I. Kwanza, Yesu Kristo Mwenyewe amedharauliwa na kukataliwa na kizazi cha mwanadamu.

Isaya aliyekuwa nabii mwinjilisti aliiweka bayana aliposema,

“Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu” (Isaya 53:3).

Dkt. Torrey alisema, “Ukosewa wa [kuwa] na imani katika Yesu Kristo si msiba, ni dhambi, dhambi ya kusikitisha, dhambi ya kuogofya, na dhambi inayoangamiza” (R. A. Torrey, D.D., Jinsi ya kumfanyia kazi Kristo, Kampuni ya Fleming H. Revell, n.d., uk. 431). Nabii Isaya aliielezea dhambi ya kumtweza na kumkataa Kristo, kama ukosefu ulio ndani unaosababisha watu waliopotea kuficha nyuso zao kwa Kristo. Thibitisho kuu la ukosefu kamili wa mwanadamu ni kwamba wanafikiria machache sana kuhusu Yesu Kristo Mwenyewe. Thibitisho kuu la wanadamu waliopotea kwamba wanastahili adhabu ya milele katika siwa la moto ni kwamba kwa makusudi na kwa mazoea wameficha nyuso zao Kwake.

Katika ile hali ya kutokuwa na uongofu wanadamu umtweza Yesu Kristo Mwenyewe. Katika hali yao ya ukosefu mkuu, hawamheshimu Yesu Kristo Mwenyewe. Hadi utakapochomwa katika dhamiri yako, hadi utakapohukumika kwa sababu ya dhambi zako, hadi utakapohisi ya kwamba mwoyo wako umekufa kumwelekea Mungu, utaendelea kumtweza na kumkataa Yesu Kristo Mwenyewe.

Katika kanisa letu tunaona hili likitendeka katika chumba cha mahojiano, baada ya mahubiri. Tunasikia watu wakisema mambo mengi. Wanazungumzia kuhusu vifungu vya Bibilia. Wanazungumzia kuhusu “kufahamu” jambo hili ama lile. wanatuambia vile wanavyohisi na vile walivyofanya. Na kila mara wanamalizia kwa kusema, “Halafu nikaja kwa Yesu.” Ni hayo tu! Hawawezi kuliongeza neno lingine hata moja kuhusu Yesu! Hawana jambo lolote la kusema kuhusu Yesu Kristo Mwenyewe! Ingewezekana aji waokolewe?

Mhubiri aliyekuwa mashuhuri aliyeitwa Spurgeon alisema, “Kuna mazoea hafifu kwa watu kumwacha Yesu Kristo Mwenyewe wanapohubiri injili” (C. H. Spurgeon, Mzunguko katika lango, Kitabu cha Msafiri, 1992 chapa ya pili, uk. 24).

Kujua utaratibu wa wokovu hakuwezi kukuokoa! Kujifundisha mengi katika Bibilia hakuwezi kukuokoa! Kusikia mahubiri mengi hakuwezi kukuokoa! Kuhisi huzuni kwa sababu ya dhambi zako hakuwezi kukuokoa! Haikumuokoa Yuda, ilimuokoa? Kuweka wakfu maisha yako hakuwezi kukuokoa! Machozi yako hayawesi kukuokoa! Hakuna chochote kinachoweza kukusaidia ila tu uongozwe kuacha kumdharau na kumkataa Yesu Kristo – ila tu uongozwe kutoficha uso wako Kwake – ila tu uvutwe kwa Yesu Kristo Mwenyewe! Imba kibwagizo hiki tena!

Yesu pekee, acha nimuone,
   Yesu pekee, hakuna mwingine ila Yeye,
Halafu wimbo wangu utakuwa milele –
   Yesu! Yesu pekee!

Mnaweza kuketi.

II. Pili, Yesu Kristo Mwenyewe ndiye mada kuu katika Bibilia yote.

Hakuna madhumuni yeyote kwetu kukuambia kwamba Yesu Kristo Mwenyewe awe kiini katika mawazo yako? Hapana, si ya kwamba haina madhumuni. Kwa nini, hebu fikiria, Yesu Kristo Mwenyewe ndiye mada kuu katika Bibilia yote – kutoka mwanzo hadi ufunuo! Baada ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu aliwakuta wanafunzi wawili wakitembea kwelekea Emmau. Alicho waambia kina umuhimu hata siku ya leo.

“Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.”
    (Luka 24:25-27).

Katika vitabu vitano vya Musa, na kuendelea katika Bibilia nzima, Kristo aliwaeleza “katika maandiko mambo yote yaliyomhusu.” Ni nini ingekuwa wazi zaidi? Mada kuu katika Bibilia nzima ni Yesu Kristo Mwenyewe! Kwa sababu Yesu Kristo Mwenyewe ndiye hoja kuu katika Bibilia, si inaweza kuwa sababu ya kutosha kumfanya Yesu Kristo Mwenyewe kuwa hoja muhimu katka mawazo yako na maisha yako? Nakwambia, fikiria kwa undani asubuhi hii kumhusu Yesu Kristo Mwenyewe! Imba kibwagizo hiki tena!

Yesu pekee, acha nimuone,
   Yesu pekee, hakuna mwingine ila Yeye,
Halafu wimbo wangu utakuwa milele –
   Yesu! Yesu pekee!

Ninaamini ya kwamba kumjua Yesu Kristo Mwenyewe, katika uongofu halisi, ndilo jambo la muhimu sana ambalo linaweza tendeka kwako. Ikiwa kwa hakika utamwamini Yesu Kristo Mwenyewe utahitaji tu ushauri kidogo. Ninaamini ya kwamba kuwa na habari sahihi kuhusu Yesu Kristo kutaondoa kwa asili mia 90% lile hitaji la ushauri wa Ukristo! Mtu anapomjua Kristo, kwa uongofu halisi, atamtambua Kristo kama,

“...aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi”
     (I Wakorintho 1:30).

Ikiwa tutaacha “uamuzi ghushi” katika makanisa yetu, tukihakikisha ya kwamba watu wamepokea kwa kweli uongofu kwa Kristo, itaondoa asili mia 90% ya ushauri unaofanywa makanisani siku hisi! Mwache Yesu Kristo Mwenyewe awe mshauri! Imba kibwagizo hiki tena!

Yesu pekee, acha nimuone,
   Yesu pekee, hakuna mwingine ila Yeye,
Halafu wimbo wangu utakuwa milele –
   Yesu! Yesu pekee!

III. Tatu, Yesu Kristo Mwenyewe ndiye kiini, chanzo asili, na moyo wa injili.

Nabii Isaya alizungumzia Yesu Kristo Mwenyewe kuwa moyo wa Injili,

“Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:6).

“Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.” Kuwa badala, kwa kifo cha Kristo cha upatanisho, mahali pako, anapolipa gharama na kupitia mateso ya ghadhabu ya Mungu mahali pako – huo ndio moyo wa Injili! Ni Yesu Kristo Mwenyewe anapozipokea dhambi zako gizani pale Gethsemane. Ni Yesu Kristo Mwenyewe pale Bustani, aliyesema,

“Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni” (Marko 14:34).

Ni Yesu Kristo Mwenyewe ambaye,

“Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini” (Luka 22:44).

Ni Yesu Kristo Mwenyewe aliyekamatwa pale Bustani ya Gethsemane. Ni Yesu Kristo Mwenyewe aliyeburutwa mbele ya Baraza, alichapwa usoni, alidhihakiwa na kufedheheshwa. Walimtemea mate usoni Yesu Kristo Mwenyewe! Walingoa baadhi ya nywele kutoka kwa kidevu cha Yesu Kristo Mwenyewe. Ni Yesu Kristo Mwenyewe aliyepelekwa mbele za Pilato, alichapwa mgongoni na mjeledi wa Warumi, alivalishwa taji ya miba, Damu ilitiririkia kwa uso uliobarikiwa wa Yesu Kristo Mwenyewe, uso Wake ulipigwa kiasi cha kutojulikana,

“uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu”
     (Isaya 52:14).

“Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” (Isaya 53:5).

Ni Yesu Kristo Mwenyewe aliyetolewa kutoka kwa ikulu ya Pilato, akiuburuta Msalaba Wake hadi mahali pa kuuliwa. Ni Yesu Kristo Mwenyewe aliyesulubishwa kwa huo mti uliolaaniwa. Ni Yesu Kristo Mwenyewe aliyeteseka si tu kupitia uchungu wa misumari iliyopigiliwa mikononi na miguuni – lakini pia alipitia uchungu mwingi zaidi wakati ambapo Mungu “ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:6). Yesu Kristo Mwenyewe “alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti” (I Petro 2:24). Dkt. Watts alisema,

Tazama, kutoka kichwani Mwake, mikononi Mwake, miguuni Mwake,
   Huzuni na upendo zilitiririka pamoja:
Upendo na huzuni wa namna hii umewahi kutana,
   ama miba kutengeneza taji nzuri vile?
(“Ninapotazama msalaba wa ajabu” na Isaka Watts, D.D., 1674-1748).

Simama na uimbe! Sasa imba kibwagizo chetu!

Yesu pekee, acha nimuone,
   Yesu pekee, hakuna mwingine ila Yeye,
Halafu wimbo wangu utakuwa milele –
   Yesu! Yesu pekee!

Mnaweza kuketi.

IV. Nne, Yesu Kristo Mwenyewe ndiye chanzo pekee cha furaha ya milele.

Waliuteremsha mwili wa Yesu kutoka kwa msalaba na wakauzika kwa kaburi iliotiwa muhuri. Lakini siku ya tatu, alifufuka kimwili kutoka kwa wafu! Halafu akaja kwa Wanafunzi Wake na akasema, “Amani iwe kwenu” (Yohana 20:19).

“Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana” (Yohana 20:20).

“Basi wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana” (Yohana 20:20).Yesu Kristo Mwenyewe aliwapa furaha “walipomwona Bwana.” Hauwezi kuijua amani ya kina, na furaha ya Bwana, hadi utakapomjua Yesu Kristo Mwenyewe!

Oo, nawambia asubuhi hii – naweza kukumbuka wakati hasa nilipomwamini Yesu Kristo Mwenyewe! wakati huo nilihisi utakatifu! Nilimkimbilia! ama, zaidi, inaonekana Alinikimbilia. Nilioshwa nikawa msafi kutokana na dhambi na damu Yake ya thamani! Nilifanywa kuwa hai na Mwana wa Mungu! Imba kibwagizo hicho tena!

Yesu pekee, acha nimuone,
   Yesu pekee, hakuna mwingine ila Yeye,
Halafu wimbo wangu utakuwa milele –
   Yesu! Yesu pekee!

Mnaweza kuketi.

Kuja kwa Yesu Kristo Mwenyewe! Usimwache Mwokozi nje ya maisha yako. Usimwache nje ya shuhuda zako. Usitende yale Spurgeon aliita “mwelekeo mbaya…kumwacha Kristo Mwenyewe nje ya injili.” Hapana! Hapana! Kuja sasa kwa Yesu Kristo Mwenyewe. Sikiliza vizuri maneno haya ninayoyaimba.

Jinsi nilivyo, bila hoja hata moja,
   Lakini siku hiyo damu yako ilimwagika kwa ajili yangu,
Na ya kwamba unaniita nije Kwako,
   Ee Mwana Kondoo wa Mungu, Naja! Naja!
(“Jinsi nilivyo” na Charlotte Elliott, 1789-1871).

Yesu alikufa msalabani kulipa deni ya dhambi zako. Yesu alimwaga damu Yake takatifu ili kuziosha dhambi zako zote. Kuja kwa Yesu. Mwamini na atakuokoa kutoka kwa dhambi zote. Amin.


UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.

(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”

Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.

Wimbo uliimbwa kabla ya mahubiri na Bw. Benjamini Kincaid Griffith:
“Asubuhi inapopamba anga” (uliotafsiriwa kutoka kwa Kijerumani na Edward Caswall, 1814-1878).


MWONGOZO WA

YESU KRISTO MWENYEWE

JESUS CHRIST HIMSELF

na Dkt. R. L. Hymers, Jr.

“Yesu Kristo Mwenyewe” (Waefeso 2:20).

I.   Kwanza, Yesu Kristo Mwenyewe alitwezwa na kukataliwa na kizazi cha mwanadamu, Isaya 53:3.

II.  Pili, Yesu Kristo Mwenyewe ndiye mada kuu katika Bibilia yote,
Luka 24:25-27; I Wakorintho 1:30.

III. Tatu, Yesu Kristo Mwenyewe ndiye kiini, chanzo asili, na moyo wa Injili,
Isaya 53:6; Marko 14:34; Luka 22:44; Isaya 52:14; 53:5; I Petro 2:24.

IV. Nne,Yesu Kristo Mwenyewe ndiye chanzo pekee cha furaha ya milele,
Yohana 20:19, 20.