Kusudi la tovuti hii ni kuandaa makala ya mahubiri na mahubiri ya video bila malipo kwa Wachungaji na Wanamisheni duniani kote, hasa katika Ulimwengu wa Tatu, sehemu ambazo kuna uchache ama ukosefu wa vyuo vya theolojia au shule za Bibilia.
Makala ya mahubiri haya na video ufikia kompyuta 1,500,000 katika zaidi ya nchi 221 kila mwaka kupitia tovuti www.sermonsfortheworld.com. Mamia ya watu wengine hutazama video kupitia You Tube, lakini wao huondoka kutoka YouTube na kuingia katika tovuti yetu. YouTube huwaelekeza watu katika tovuti yetu. Makala ya mahubiri haya yanatolewa kwa lugha 46 kwa kompyuta takriban 120,000 kila mwezi. Makala ya mahubiri haya hayana hatimiliki, hivyo wahubiri wanaweza kuyatumia bila idhini yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili ujue jinsi unavyoweza kutuma mchango wako kila mwezi ili utusaidie katika kazi hii kuu ya kueneza Injili kote ulimwenguni.
Kila unapomwandikia Dkt. Hymers kila wakati mjulishe nchi unayoishi, la sivyo hawezi kukujibu. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net.
UFALME WA MILENIATHE MILLENNIAL KINGDOM na Dkt. R. L. Hymers, Jr. “Basi nanyi salini hivi: Baba yetu aliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” (Mathayo 6:9-10). |
Kwa karibu miaka elfu mbili Wakristo wameomba “Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbingun.” Tunaomba “Sala ya Bwana” kila tunapomaliza ibada yetu kama jamii katika nyumba yetu kila usiku. Wengine wanaweza kusema tu ni kawaida ya dini, lakini kwangu binafsi ni ombi kamilifu na umaanisha kila neno katika sala hii. Nyanyangu mkongwe, mamake mamangu, aliomba “Sala ya Bwana” nami kila usiku nilipokuwa mvulana mdogo, na nimeendelea kufanya hivyo maisha yangu yote, kila usiku kabla sijalala. Dkt. J. Vernon McGee alisema,
“Ufalme wako uje” ndio ufalme ambao Mathayo amekuwa akiuzungumzia, ufalme ambao Kristo atahuanzisha katika hii dunia. Hili ni ombi muhimu kila mmoja wetu anastahili kuomba (J. Vernon McGee, Th.D., Kupitia Biblia, Kilichochapishwa naThomas Nelson, toleo la 1983, sehemu ya IV, uk. 37; maelezo kuhusu Mathayo 6:10).
Ninapoomba ombi hilo, Ninaomba Ufalme wa Milenia uje kwa ukamilifu Kristo atakaporudi. Neno “milenia” linamaanisha elfu moja. Neno la Kiyunani “chilia” (elfu moja) limetumika mara sita katika Ufunuo 20:2-7. Wakristo wa karne ya kwanza na ya pili waliamini kutakuwa na utawala halisi wa miaka 1,000 wa Kristo katika dunia hii. Waliamini milenia ni ya wakati ujao. Hiyo ina maana kwamba Wakristo wa kale walitarajia Kristo atarudi duniani kuanzisha Ufalme wake. “Imani ya kuwa na milenia” ina maanisha ya kwamba Kristo atarudi kabla ya milenia kuanzisha Ufalme wake kwa miaka elfu moja. Papias (alifariki A.D. 165) alisema, “Kutakuwa na milenia baada ya ufufuo wa wafu, wakati utawala halisi wa Kristo utaanzishwa katika dunia hii.” Polycarp (A.D. 70-156) alizungumzia kuhusu [Wakristo] kutawala pamoja na Kristo na kuhusu ukweli kwamba watakatifu watahukumu ulimwengu (tazama Henry C. Thiessen, Ph.D., Mafundisho ya Utangulizi Katika Theolojia ya Utaratibu, Kampuni ya uchapishaji ya Eerdmans, toleo la 1949, uk. 470).
Lakini muda ulipokuwa ukiendelea baadhi ya Wakristo mashuhuri walianza kufundisha ya kwamba Ufalme ni mfamo ulio katika fumbo na si Ufalme halisi. Walianza kufundisha ya kwamba hakutakuwa na Milenia, Mafundisho haya yalianza na Clement wa Alexandria (A.D. 155-220) na hasa Origen wa Alexandria (A.D. 185-254). Mafundisho yao, yaliyoleta dhana kwamba Ufalme wa miaka 1,000 ni katika mfano na mafumbo na dhana hii ni ya kiroho na si halisi yalifanikiwa, na baraza la Roma chini ya Papa Damasus walikataa mtazamo wa Milenia ya wakati ujao, na mafundisho haya wakayaita “mafundisho ya elfu moja,” katika mwaka wa A.D. 373. Hivyo, Kanisa la Katoliki likawa haliamini kutakuwa na Milenia, yaani, walifundisha ya kwamba Kristo hatarudi kuanzisha Ufalme hapa duniani, na kwamba Kanisa la Katoliki polepole litabandilisha ulimwengu, na ahadi za Ufalme zitatimizwa kupitia ushindi wa Ukatoliki. Mtazamo huu ni ule wa dhana kwamba “hakuna Ufalme utakaokuja duniani.” Yaani hakutakuwa na Ufalme wa Milenia hapa duniani.
Daniel Whitby (A.D. 1638-1726) alikuwa mtu ambaye haamini Utatu, aliamini Umoja na alisema Kristo si Mungu. Whitby alirejesha ile dhana kwamba Milenia ni mfano na mafumbo iliyokuwa ya Origen, lakini akaiita “hali ya kudhani upya.” Daniel Whitby, Mzushi wa Umoja aliyekataa Utatu, “alifundisha ya kwamba ahadi zote za Ufalme zinastahili kuchukuliwa kwa njia ya kiroho na ya mfano na mafumbo…Mara nyingi anaitwa baba wa dhana ya kisasa ya kwamba Kristo atarudi baada ya milenia” (Thiessen, uk. 471). Mafundisho haya yanafundisha kwamba Kristo atarudi baada ya milenia – baada ya kanisa kubadilisha kiasi kikubwa cha ulimwengu. Dhana hii ya kwamba Kristo atarudi baada ya kanisa kubadilisha ulimwengu, kwa hakika, ni njia tu ya kisasa ya kusema hakutakuwa na milenia. Wanaamini ya kwamba hakutakuwa na urejesho wa Israeli sawasawa na wanavyoamini wanaosema hakutakuwa na milenia, ya kwamba “kanisa” litachukua mahali pa Israeli, na kwamba Kristo hatarudi kwa njia inayoonekana kuanzisha Ufalme Wake, na ya kwamba “ kanisa” litabadilisha ulimwengu, na kuleta kipindi cha kupendeza duniani. Mal Couch alisema,
Vita vya Dunia vya kwanza, na mwishowe Vita vya Dunia vya pili, kwa kweli vilitamatisha matumaini ya wanaoamini kwamba milenia ni wakati huu. Ukatili wa mwanadamu ulionekana wazi na mambo hayakuonekana yakienda vizuri, kama [walivyo] fundisha (Mal Couch, Ph.D., Biblia ya kinabii ya kujifundisha ya Tim LaHaye, Wachapichaji wa AMG, 2000, uk. 1398).
La kushangaza, hii dhana ya mfano na mafumbo, inayotazama mambo kwa njia ya kiroho inaonekana ikirejea, kwa njia ya “theolojia ya mabadilisho” [“kanisa” likichukua mahali pa Israeli katika mpango wa Mungu] na kudai ya kwamba “kanisa” linaweza “kushinda jamii na kurejesha haki” na kuanzisha Ufalme (Couch, ibid.). Hii kwa hakika ni kurejelea ule mtazamo wa Katoliki wa Ukristo wa “kushinda” na “kubadilishana” Wayahudi na “kanisa” katika mpango wa Mungu. Hivyo sivyo Biblia inavyofundisha.
Nilisomea katika Chuo cha Theolojia cha Golden Gate Baptist Theological Seminary (Baptisti ya Kusini) wakati kilikuwa bora kuliko kilivyo leo. Namkumbuka profesa mmoja aliyefundisha mafundisho kwamba hakutakuwa na ufalme wa milenia na pia kwamba milenia ni wakati huu wa kanisa na walifundisha kana kwamba ni ukweli. Halafu alidhalilisha na kudhihaki dhana kwamba kutakuwa na Ufalme wa Milenia halisi, akiyaita “mafundisho ya elfu moja,” na uzushi, na kuyadhalilisha kama mafundisho ya uwongo yanayofundishwa na Biblia ya kujifundisha ya Scofield, lakini hayaaminiwi na “wasomi.” Alishambulia Biblia ya kujifundisha ya Scofield kuhusu mada hii mara nyingi, hata nikaenda nikainunua mara ya kwanza – na nimeitumia kutoka wakati huo! Ninahubiri kutoka kwa Biblia ya kujifundisha ya Scofield jioni ya leo, kama ninavyofanya kila Jumapili, kwa sababu ninaamini Kristo atarudi kabla ya milenia kama inavyofundishwa katika Biblia ya kujifundisha ya Scofield. Nina uhakika ya kwamba Biblia haifundishi kwamba hakutakuwa na milenia halisi au Kristo atarudi baada ya milenia.
Jumapili iliyopita tuliona aina tatu za ukweli uliomkuu katika Zekaria 14:4-5, 9. Kwanza, Kristo atarudi ghafla katika Mlima wa Mizeituni,
“Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki…” (Zekaria 14:4).
Kristo atarudi kutoka mbinguni, atarudi tu katika ule Mlima wa Mizeituni mahali alipokuwa alipopaa juu. Malaika walisema,
“Wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato” (Matendo ya Mitume 1:11-12).
“Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni” (Zekaria 14:4). Miguu ile ile iliyochomwa na misumari msalabani itarudi katika ule mlima tu ambapo Kristo alikuwa alipopaa kurudi mbinguni (Matendo ya Mitume 1:9-12). Pili, Kristo atarudi pamoja na watakatifu wake wote.
“Na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye” (Zekaria 14:5).
Hii inamaanisha kwamba Wakristo walionyakuliwa watateremka kutoka angani, wakimfuata Kristo. Tukio hili lilitabiriwa na Henoko kabla ya gharika.
“Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu” (Yuda 14).
Na Mtume Yohana alizungumzia haya katika Ufunuo 19:14, “Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata,” atakapokuwa akirudi kutoka Mbinguni kuliaribu jeshi la Mpinga Kristo na kuanzisha ufalme wake wa miaka elfu moja hapa duniani. Tatu, Zekaria 14:9 inasema ya kwamba ndipo Kristo ataanzisha Ufalme wake duniani,
“Naye BWANA atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja” (Zekaria 14:9).
Na mwishowe maombi ambayo yameombwa kwa miaka elfu mbili yatajibiwa,
“Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” (Mathayo 6:10).
Mwishowe, tuliangalia Ufunuo 20, na ninataka tufungue hapo tena usiku wa leo. Tafadhali fungua Ufunuo 20, kuanzia mstari wa kwanza. Hapa tunajifundisha ukweli aina mbili muhimu kuhusu Ufalme unaokuja.
I. Kwanza, Shetani atafungwa miaka 1,000.
“Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu, akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache” (Ufunuo 20:1-3).
Utaona ya kwamba “miaka elfu” imetajwa mara mbili kutoka mstari wa kwanza hadi wa tatu. “Miaka elfu” imetajwa kwa jumla mara sita katika sura ya kumi na mbili katika kitabu cha Ufunuo. Dkt. McGee alisema,
Ni ukweli kwamba Milenia imetajwa katika sura moja tu, lakini Mungu aliitaja mara sita [katika hiyo sura]. Ni mara ngapi anastahili kusema jambo kabla halijakuwa ukweli? Anataja mambo mengine ambayo watu wanasisitiza na kufikiria ni ya muhimu kwa sababu tu yanapatikana mara moja ama mara mbili kwa Maandiko. Miaka elfu imetajwa mara sita, na hapa imetajwa kuhusiana na Shetani (McGee, ibid., sehemu ya 5, uk. 1055; maelezo kuhusu Ufunuo 20:1-3).
Kutokuwa kwa Shetani duniani wakati wa Ufalme wa Milenia kutabandilisha hali kutoka kwa giza hadi kwa nuru. Muda ule wote Shetani atakuwa akifanya kazi hapa duniani haiwezekani kuwa na Ufalme kamilifu. Mapenzi ya Mungu hayawezi timia “hapa duniani, kama huko mbinguni” (Mathayo 6:10) wakati wote ambapo Shetani atakuwa huru katika dunia hii.
Malaika atateremka na nyororo kubwa na atamfunga Shetani kwa kipindi chote cha Ufalme wa Milenia wa Kristo.
“Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu, akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache” (Ufunuo 20:1-3).
Shetani atatupwa “katika kuzimu, na atafungwa” (Ufunuo 20:3) wakati wa Ufalme wa Kristo wa miaka elfu. Shetani atafungwa “katika kuzimu,” hasa “shimo kubwa.” Hii siyo ziwa la moto. Shetani atatupwa katika Ziwa la Moto baada ya Ufalme kufika tamati, mwisho wa miaka elfu. Itakuwa dunia ya ajabu aji wakati Kristo ataanzisha Ufalme wake hapa duniani. Shetani hatakuwa hapa kutujaribu na kututesa tena katika Ufalme wa Mungu wetu na Kristo wake! Kama vile wimbo wa zamani unavyosema,
Utawala wa Shetani u karibu kufika kikomo,
Oo, ingekuwa aji kwamba ingekuwa ni leo!
Huzuni na kite hazitakuwa tena,
Oo, ingekuwa aji kwamba ingekuwa ni leo!...
Utukufu, utukufu! itakuwa furaha katika moyo wangu.
Utukufu, utukufu! Wakati [Mungu] atakapomtawaza kuwa Mfalme.
Utukufu, utukufu! kwa haraka tayarisha njia;
Utukufu, utukufu! Yesu atarudi siku moja.
(“Ingekuwa aji kama ingekuwa ni leo?” na Lelia N. Morris, 1862-1929;
na kufanyiwa mageuzi na Mchungaji).
Shetani atafungwa katika kuzimu kwa kipindi chote cha Ufalme! Ni ahadi ya ajabu aji!
II. Pili, halafu Ufalme wa Kristo utaanzishwa duniani kwa miaka elfu moja.
Tafadhali soma nami katika Biblia yako ninaposoma Ufunuo 20:4-6.
“Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. Hao watu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu” (Ufunuo 20:4-6).
Biblia ya kinabii ya kujifunza ya LaHave inasema ya kwamba mstari wa nne na wa tano inazungumzia wale ambao watauawa na Mpinga Kristo wakati wa dhiki kuu kwa kukataa kupokea chapa yake katika mikono yao au vipaji vya nyuso zao. Watafufulia kimwili ili waweze kutawala pamoja na Kristo wakati wa Ufalme wake wa miaka elfu moja duniani (tazama Biblia ya kinabii ya kujifunza ya Tim LaHave, Wachapishaji wa AMG, toleo la 2000, uk. 1399; maelezo kuhusu Ufunuo 20:4-5). Mstari wa sita unasema,
“ Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu” (Ufunuo 20:6).
Biblia ya kinabii ya kujifunza ya Tim LaHave inasema hivi kuhusu huu mstari,
“Ufufuo wa kwanza” ni wa waaminio na utatendeka kwa sehemu tatu: (1) Kristo kama malimbuko (I Kor. 15:20); (2) unyakuzi…(I Kor. 15:23; I The. 4:13-18); (3) Watakatifu wa dhiki kuu wanafufuliwa kabla ya Ufalme wa Milenia pamoja na watakatifu wa Agano la Kale (Zaburi 50:1-6). Ufufuo huu unajumlisha wafu wote ambao [waliongoka] hadi wakati wa kurudi kwa Kristo (ibid., uk. 1400; maelezo kuhusu Ufunuo 20:6).
Mstari wa sita unaonyesha ya kwamba wanaofufuliwa “katika ufufuo wa kwanza,”
“Watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu” (Ufunuo 20:6).
Litakuwa jambo nzuri aji kutawala pamoja na Kristo katika Ufalme wake! Lakini lazima tuwe washindi ili tupate kufanya hivyo. Tunasoma katika Ufunuo 3:21,
“Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi” (Ufunuo 3:21).
Kufaulu ili utawale pamoja na Kristo katika Ufalme wake duniani, ni lazima uwe mshindi. Lakini kuwa mshindi, ni lazima kwanza uongoke. Yesu alifafanua wasi kwamba hatua ya kwanza ya kuingia na kutawala katika Ufalme ni uongofu halisi. Yesu alisema,
“Msipoongoka na kuwa kama vitoto hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 18:3).
Lazima upokee uongofu wa kweli la sivyo hautaingia katika “ufalme wa mbinguni,” na ikiwa hautaingia “ufalme wa mbinguni” kwa hakika hautaingia katika Ufalme wa Kristo wa miaka elfu moja duniani! Kwa hivyo, ni lazima utafute uongofu wa kweli katika Kristo kuliko mambo mengine yote katika maisha!
Uongofu halisi kwa kawaida uhusisha kule kuhukumika na dhambi kwanza, halafu unaanza kujitahidi kujiokoa kutokana na dhambi hadi unapogundua ya kwamba hauwezi. Mwishowe, uongofu unapatikana unapokata tamaa katika juhudi zako, unapogundua ya kwamba umepotoka kabisa, na halafu unakuja kwa Kristo ili utakazwe kutokana na dhambi zako na Damu Yake. Unapokuja kwa Kristo dhambi zako zimelipiwa kupitia kifo chake msalabani. Unapokuja kwa Kristo aliyefufuka na aliye mbinguni, na upate pumuziko kwake kwa imani pekee, utapata uongofu wa kweli na utaanza kuwa mshindi, ambaye amefaulu kutawala pamoja na Kristo katika Ufalme wake wa Milenia hapa duniani. Lakini hatua ya kwanza ni kutafuta uongofu halisi katika Kristo Yesu. Na Mungu hivi karibuni akupe uongofu katika Yesu Kristo. Amina.
UNAPOMWANDIKIA DKT. HYMERS NI LAZIMA UMWAMBIE UNAANDIKA KUTOKA NCHI GANI AU HATAJIBU BARUA PEPE YAKO. Ikiwa mahubiri haya yatakubariki tuma barua pepe kwa Dkt. Hymers na umwambie lakini kila mara mjulishe unaandika kutoka nchi gani. Barua pepe ya Dkt. Hymers ni rlhymersjr@sbcglobal.net (bonyeza hapa). Unaweza kumwandikia Dkt. Hymers kwa lugha yeyote, lakini andika kwa kingereza ikiwa unaweza. Ikiwa unataka kumwandikia Dkt. Hymers kupitia posta, anwani yake ni S.L.P. 15308, Los Angeles, CA 90015. Unaweza kumupigia simu kupitia nambari hii (818)352-0452.
(MWISHO WA MAHUBIRI)
Unaweza soma mahubiri ya Dkt. Hymers kila wiki kwa Tovuti
hii www.sermonsfortheworld.com.
Bonyeza hapa kwa “Mahubiri kwa Kiswahili.”
Maandishi ya mahubiri haya hayana hatimiliki. Unaweza kuyatumia bila ruhusa ya
Dr. Hymers. Hata hivyo, mahubiri yote ya video ya Dkt. Hymers, na mahubiri mengine yote
ya video kutoka kwa kanisa yetu, yako na hatimiliki na yanaweza tumiwa tu kwa kuuliza ruhusa.
Wimbo ulioimbwa kabla ya mahubiri:
“Ingekuwa aji kama ingekuwa ni leo?” (na Lelia N. Morris, 1862-1929).
MWONGOZO WA UFALME WA MILENIA THE MILLENNIAL KINGDOM na Dkt. R. L. Hymers, Jr. “Basi nanyi salini hivi: Baba yetu aliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” (Mathayo 6:9-10). (Zekaria 14:4; Matendo ya Mitume 1:11-12; Zekaria 14:5; I. Kwanza, Shetani atafungwa miaka 1,000, Ufunuo 20:1-3. II. Pili, halafu Ufalme wa Kristo utaanzishwa duniani kwa miaka elfu moja, Ufunuo 20:4-6; 3:21; Mathayo 18:3. |